Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Dkt. Doto Biteko, amewataka wananchi kuendelea kudumisha umoja, mshikamano na amani kwa maslahi ya Taifa.
Wito huo umetolewa leo Januari 12, 2026, wakati akitoa salamu za heri kwa wananchi wa Jimbo la Bukombe na Watanzania wote kwa ujumla, katika kuadhimisha miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo Januari 12.
Dkt. Biteko amesema Mapinduzi ya Zanzibar ni nguzo muhimu ya haki, usawa na utu wa Mtanzania, yaliyoasisi safari ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi, sambamba na kuimarisha umoja wa kitaifa, mshikamano na amani nchini.
Aidha, amewahimiza Wanachi wema wa Bulombe kuendelea kuwa walinzi wa amani na wazalendo wa kweli kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo, huku wakithamini historia, misingi na tunu za Taifa.
Kwa upande wake, mkazi wa Ushirombo, Mathias John, akipokea salamu hizo, amempongeza Dkt. Biteko kwa uongozi wake mzuri na kwa kuendelea kuwajali na kuwapenda wananchi wa Jimbo la Bukombe.

Comments
Post a Comment