CAF YAMFUTA MWAMUZI ALIYECHEZESHA TAIFA STARS NA MOROCCO AFCON 2025


Na, Mwandishi Wetu

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limewaondoa baadhi ya waamuzi waliokuwa wakichezesha mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, kufuatia tathmini ya kina ya viwango vyao vya usimamizi wa mechi, huku likiendelea kuwafanyia tathimini waamuzi wengine waliosalia.Miongoni mwa waamuzi walioondolewa ni Boubou Traoré, aliyesimamia mechi ya hatua ya 16 bora kati ya wenyeji Morocco na Tanzania (Taifa Stars). Traoré hataendelea kupewa nafasi ya kuchezesha mechi nyingine za AFCON 2025 baada ya tathimini kubaini kuwa kiwango chake hakikidhi vigezo vilivyowekwa na CAF.Aidha, CAF pia imemwondoa mwamuzi Abdou Abdel Mefire raia wa Cameroon, aliyesimamia mechi ya hatua ya 16 bora kati ya Nigeria na Msumbiji.

Uamuzi huo umetokana na tathimini ya kitaalamu ya CAF inayolenga kuboresha ubora wa usimamizi wa mashindano hayo, ambapo shirikisho hilo limesisitiza dhamira yake ya kuhakikisha mechi zinaendeshwa kwa haki, uwazi na kuzingatia viwango vya juu vya soka barani Afrika.

Comments