Na, Ernest Magashi
Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Dkt. Doto Mashaka Biteko, leo Novemba 11, 2025, ameapishwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Kumi na Tatu, kilichofanyika jijini Dodoma.
Baada ya kula kiapo hicho, wananchi wa Wilaya ya Bukombe wamempongeza Mbunge wao kwa hatua hiyo muhimu, wakieleza matumaini yao kwamba ataendelea kutekeleza kwa vitendo Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwaletea maendeleo endelevu katika nyanja mbalimbali.
Pius Mulekwa, mkazi wa Ilyamchele, Ushirombo, alisema wanampongeza Dkt. Biteko kwa uaminifu na utendaji wake uliotukuka, na wanaendelea kumwombea kwa Mungu ili aendelee kuwatumikia wananchi kwa moyo wa upendo na uadilifu.
Kwa upande wake, Neema Samwel, mjasiriamali mkazi wa Ushirombo, alisema wananchi wanamwamini na wanampenda Dkt. Biteko kutokana na bidii yake katika kusukuma mbele maendeleo ya Bukombe.
Baada ya kula kiapo hicho, wananchi wa Wilaya ya Bukombe wamempongeza Mbunge wao kwa hatua hiyo muhimu, wakieleza matumaini yao kwamba ataendelea kutekeleza kwa vitendo Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwaletea maendeleo endelevu katika nyanja mbalimbali.
Pius Mulekwa, mkazi wa Ilyamchele, Ushirombo, alisema wanampongeza Dkt. Biteko kwa uaminifu na utendaji wake uliotukuka, na wanaendelea kumwombea kwa Mungu ili aendelee kuwatumikia wananchi kwa moyo wa upendo na uadilifu.
Kwa upande wake, Neema Samwel, mjasiriamali mkazi wa Ushirombo, alisema wananchi wanamwamini na wanampenda Dkt. Biteko kutokana na bidii yake katika kusukuma mbele maendeleo ya Bukombe. Aliongeza kuwa wanamuombea afya njema na hekima zaidi ili aweze kutekeleza majukumu yake ya kila siku kwa ufanisi na kwa manufaa ya wananchi wote.

Comments
Post a Comment