WATEJA 384 WAHUDUMIWA NA MADAKITARI BINGWA HOSPIATLI YA WILAYA


Na, Mwandishi wetu

Wateja 384 wanehudumiwa na madaktari bigwa katika hospitali ya wilaya mkoani Geita kwa mada wa siku tano huku wateja wakishukru kwa hudima walioipata na Serikalini ya awamu ya sita. Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhadisi Paskas Mragili wakati akishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka timu ya Madaktari Bingwa katika Hospitali ya Wilaya ya Bukombe, hatua iliyosaidia wananchi wengi kupata huduma za kibingwa kwa gharama nafuu na bila kulazimika kusafiri umabri mrefu.Aidha, Wananchi wa Bukombe nao wameishukuru Serikali kwa kuwaletea huduma hizo, wakieleza kuwa ujio wa Madaktari Bingwa wa Mama Samia umeokoa muda na gharama walizokuwa wakitumia kufuata huduma katika hospitali za mbali kama Bugando na Chato.Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya.  Dkt. Deograsia Mkapa alisema ujio wa Madaktari Bingwa umeongeza ujuzi kwa wataalam wa afya na kuboresha huduma zinazotolewa hospitalini hapo.“Elimu tuliyoipata kutokana na ujio wa Madaktari Bingwa wa Mama Samia itaboresha utendaji kazi wetu na huduma kwa wananchi katika Hospitali ya Wilaya,” alisema Dkt. Mkapa.

Kiongozi wa timu ya Madaktari Bingwa wa Mama Samia, Dkt. Emmanuel Chogo, ameishukuru Halmashauri ya Bukombe kwa mapokezi mazuri na ushirikiano mkubwa uliooneshwa wakati wa utoaji wa huduma hizo.“Tumefurahishwa na mapokezi mazuri kutoka kwa uongozi waa halmashauri na mwitikio mkubwa wa wananchi waliojitokeza kupata huduma,” alisema Dkt. Chogo.Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Bukombe, Dkt. Yohana Fumbuka,Hospitali ya Wilaya ya Bukombe, ilipokea timu ya Madaktari Bingwa sita wa Mama Samia kwa ajili ya kufanya kliniki maalum kuanzia Oktoba 20 hadi 24, 2025 kwa lengo la Kutoa huduma za kitabibu za kibingwa kwa wananchi pamoja na mafunzo kwa vitendo kwa wataalam wa afya wa hospitali.

Timu hiyo ilijumuisha Daktari Bingwa wa Watoto (Pediatrician), Daktari Bingwa wa Afya ya Akina Mama (Gynaecologist), Daktari Bingwa wa Upasuaji (Surgeon) na Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno (Dentist)Wengine ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani (Physician) na Daktari Bingwa wa Dawa za Usingizi (Anesthesiologist)

Huduma zilitolewa kwa ushirikiano kati ya Madaktari Bingwa na wataalam wa afya wa Hospitali ya Wilaya ya Bukombe, ambapo wananchi walipata huduma za upasuaji, afya ya uzazi, watoto, kinywa na meno, pamoja na tiba za magonjwa ya ndani kama kisukari, shinikizo la damu na mengineyo.

“Kufikia Oktoba 24, 2025, jumla ya wateja 384 walihudumiwa kupitia kliniki hiyo ambapo kati yao Wateja 378 walipata matibabu kamili katika hospitali ya wilaya na Wateja saba walipatiwa rufaa kwenda Hospitali za Bugando na Chato kwa matibabu zaidi.

Pia, katika kipindi hicho cha siku tano, hospitali ilifanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 20 kutokana na huduma za kibingwa zilizotolewa.

Dkt. Yohana Fumbuka, alibainisha mafanikio ya yaliyotokana na zoezi hilo kuwa ni pamoja na Wataalam wa afya 132 wa hospitali ya wilaya walipata mafunzo ya vitendo na nadharia, hivyo kuimarisha uwezo wao katika kutoa huduma bora kwa wananchi.

Zoezi hili ni kielelezo cha dhamira njema ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa ngazi zote nchini.

Comments