WALIMU BUKOMBE KUSHEREKEA SIKU YAO KESHO


Na Henry Evarist

Mwenyekiti Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Bukombe Ramadhan Mng'oi amewaita walimu wote na wananchi wa wilaya ya Bukombe kusherekea Siku ya Mwalimu Duniani katika viwanja vya shule ya Sekondari Ushirombo Oktoba 3, 2025.

Mng’oi ameweka wazi kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya mwaka huu ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na kuwa pamoja na burudani za mchana, kutakuwa na “Usiku wa Mwalimu” (mkesha wa burudani kwa walimu na wananchi wote.

Zaidi ya watu 6,000 wanatazamiwa kushiriki tukio hilo linalodhaminiwa na bank ya CRDB Tanzania kwa kushirikiana na Chama cha Walimu Bukombe, KNK. Jembe Ni Jembe FM na halmashauri ya wilaya ya Bukombe.

Wageni waalikwa siku ya mwalimu duniani ni pamoja waratibu kata na tarafa, viongozi wa chama cha walimu (CWT), walimu wastaafu, wasanii, wazee maarufu, wakuu wa idara halmashauri ya wilaya ya Bukombe, viongozi wa dini, tiba asili, madiwani, viongozi ccm (w), wakuu wa vitengo TSC, uthibiti ubora, elimu msingi na sekondari, маhakама, TALGHWU, TUGHE, wadau na watendaji wa kata 17.

Pia kuna watumishi CWT, wakurugenzi, DE-O msingi na sekondari, wakuu wa wilaya, katibu tawala wilaya, TSC taifa, CCM (M) viongozi walemavu, TARURA, ruwasa, nida, tanesco, TFS, madini na walimu toka halmashauri jirani. Wengine ni TRA, wakufunzi chuo cha ualimu - Singida, walimu wa mwanza, ofisi ya REO, wenyeviti na wakuu wa mikoa jirani na Geita na wananchi wote.

Katika kuhakikisha maadhimisho hayo yanatimiza malengo ya mwanzilishi wake, Dkt. Doto Biteko ya kumheshimisha mwalimu na kumuongezea morali ya kazi katika kuinua taaluma na watoto ambao anaamini urithi pekee ni elimu, waandaaji na kamati imepanga kutoa zawadi mbali mbalimbali kwa makundi kadhaa ya walimu kupitia mashindano kama;

Kwaya bora, shindano la RAP (Freestyle), Karaoke,shindano la Dancing kwa wanaume na wanawake, Panalty Shootout (Men), Netball Shootout (Women), Ball Header Game, Dress Like a Student Talent show (Women)Dress Like a Student Talent show (Men).

Mbali na hao, kutakuwa na Wasanii Magambo Machimu, Elizabeth Maliganya, Brother K na Dogo paten ni kati ya wengine wengi.Akizungumza na kamati ya maandalizi Septemba 29, 2025 katika viwanja vya CCM wilaya ya Bukombe, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko aliitaka kamati kuhakikisha inafanyakazi kwa weledi hili walimu waifurahie siku yao.

“Makundi mbalimbali yamekuwa yakitambuliwa na kupewa heshima duniani na mataifa yote kwa kutengewa siku yao maalumu ikiwemo siku ya unuonyeshaji, siku ya wazee. UKIMWI, wanawake, wanaume, watoto nk. Walimu pia wanahaki ya kusherekea siku yao kwa furaha huku wakitathimini wajibu wao katika maendeleo ya jami” alisema.

Mwakilishi wa Bank ya CRDB, Joselin Kamuhanda amewahakikishia walimu wa wilaya ya Bukombe kuwa maadhimisho ya Siku ya Mwalimu wilayani Bukombe mwaka huu yatakuwa ya tofauti.

“Tumeandaa burudani mbalimbali mchana na usiku zikiwemo fataki, muziki mzuri kutoka Jembe ni Jembe FM, vinywaji na wasanii wenye hadhi ya kimataifa” alisema Chief Organizer Joseline.

Siku ya mwalimu duniani imekuwa ikiadhimishwa kila mwaka wilayani Bukombe tangu Mwalimu Doto Biteko alipochaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Bukombe na kuonesha matokeo chanya jambo ambalo limevutia wafadhili mbalimbali.

Wilaya ya Bukombe inaongoza katika mkoa wa Geita matokeo ya mitihani ya kitaifa kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari ambapo kitaifa ni kati ya shule 20 bora kidato cha sita.

Aidha, wilaya hiyo inaongoza kuwa na shule nyingi za kidato cha tano na sita jambo ambalo linatajwa kama upendeleo maalum wa Dkt. Samia katika awamu yake ya sita bila kutaja sekta nyingine.

Ni wilaya ambayo asilimia 80 ni pori na asilimia 20 ni maeneo ya makazi ya watu, machimbo ya dhahabu, mialo, ofisi na sehemu ya kuchunga mifugo.

Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ni moja kati ya Halmashauri tano (05) zinazounda Mkoa wa Geita, ina ukubwa wa eneo la kilometa za mraba 8,055.59.Halmashauri hii Ilianzishwa Julai mwaka 1995 kwa tangazo la serikali Na.205 la mwaka 1998 ambapo Baraza la Halmashauri ya Wilaya liliundwa rasmi mwaka 2000 baada ya uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Kwa upande wa Mashariki na Kaskazini Wilaya ya Bukombe inapakana na Wilaya ya Mbogwe, Kaskazini Magharibi inapakana na Wilaya ya Chato, upande wa Magharibi inapakana na wilaya ya Biharamulo, na kwa upande wa kusini inapakana na Wilaya ya Urambo.

Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ina tarafa 3 ambazo ni Ushirombo,Siloka, na Bukombe. Ina kata kumi na saba (17) ambazo ni Iyogelo, Busonzo, Bukombe, Butinzya,Bulega, Runzewe Mashariki, Runzewe Magharibi, Namonge, Katente, Igulwa,Bulangwa, Ushirombo, Uyovu, Bugelenga, Lyambamgongo, Katome, na Ng’anzo.

“Ukiwa na watoto wawili, mmoja ana kabutura imechanika matakoni na mwingine hana kabisa, utaanza kumnunulia ambaye hana kabisa. Tumejenga shule kwanza ambapo hakukuwa na shule kabisa huku wanafunzi wakilazimika kutembea umbali mrefu zaidi” amesema Dkt. Biteko kwenye mikutano ya kampeni kuomba kuchaguliwa tena 2025.

Siku ya Mwalimu Duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 5 Oktoba. Siku hii lianzishwa mwaka 1994 na UNESCO kwa kushirikiana na Shirikisho la Walimu Duniani (Education International).

Siku hii inakumbusha kutangazwa kwa Mapendekezo ya 1966 ya UNESCO/ILO kuhusu Hali ya Walimu, ambayo yalitoa miongozo ya kimataifa juu ya haki, wajibu na hadhi ya walimu.

Lengo kuu ni Kutambua mchango mkubwa wa walimu katika elimu na jamii, Kuelimisha umma kuhusu changamoto walizokuwa nazo walimu, Kuhimiza serikali na jamii kuboresha mazingira ya kazi, mishahara na heshima kwa walimu.

#WALIMU WETU, FAHARI YETU #KNK

Comments