VIJANA WAASWA KUJIELIMISHA ZAIDI NAMATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII


Na, Mwandishi wetu

Vijana watakiwa kujielimisha zaidi matumizi ya mitandao ya kijamii wilayani Bukombe mkoanGeita (Social Media). Wito huo umetolewa na Henry Evarist  toka Bukombe Sasa Media wakati akitoa semina ya mawasiliano, habari na matumizi ya mitandao ya kijamii kwa vijana wa parokia ya Bikira maria msaada wa Daima Ushirombo. 

Katika semina hiyo iliyofanyika leo Oktoba 5, 2025 katika ukumbi wa mafunzo parokiani hapo, Evarist ameeleza kuwa kwa mujibu wa Kamusi ya Merriam Webster 2022, Mawasiliano ni kubadilishana taarifa kati ya mtu na mtu au mtu na kikundi cha watu. Vyombo vya habari kwa upande mwingine vinafafanuliwa kama njia ya mawasiliano ambayo kwasisi tunapata habari na habari ambayo ungetaka kumsimulia rafiki kabla simu haijaishiwa bando au chaji.Mkufunzi huyo wa vijana, alitoa mwanga namna washiriki wa mafunzo na wafanyakazi wengine wanaohusika katika juhudi za ujenzi wa amani kuwa wanaweza kubadili namna ya kutumia taarifa kwa kutoa uelewa na kujenga maarifa katika mandhari au majukwaa ya vyombo vya habari vya leo na namna watakavyopenya katika vyombo vya habari, ushirikiano na mahusiano na namna ya kupambana na taarifa zisizo sahihi za vyombo vya habari.

Akiwa mshiriki wa majadiliano ya kuleta amani katika nchi za maziwa makuu, Mhariri Evarist amewasimulia washiriki ambavyo Vyombo vya habari ni mhusika muhimu katika kuchochea migogoro na kujenga amani.



 
 

Comments

  1. Hongera saana kwa Elimu hiyo kwa ajili ya vijana,maana kijana mmoja akipata Elimu vizuri nae atawaelimisha wengine

    ReplyDelete

Post a Comment