MJUE MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA BUKOMBE DKT. DOTO MASHAKA BITEKO


Na, Ernest Magashi

Dkt. Doto Mashaka Biteko ni jina linalotajwa kwa heshima kubwa katika siasa za Tanzania, hasa katika jimbo la Bukombe, mkoa wa Geita. Amezaliwa tarehe 30 Desemba, 1978 na ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).Elimu na Maisha ya Awali Safari yake ya elimu ilianza mwaka 1988 katika Shule ya Msingi Nyaruyeye hadi mwaka 1994. Aliendelea na elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Sengerema kati ya mwaka 1995 hadi 1998.Baadaye, Dkt. Biteko alipata cheti cha Ualimu Daraja la IIIA kutoka Chuo cha Ualimu Katoke, wilayani Muleba, Kagera (1999 hadi 2001), kisha kujiunga na Chuo cha Ualimu Butimba, Mwanza (2002 hadi 2004), ambako alisomea Theatre Arts.Aliendeleza taaluma yake ya ualimu kwa kupata Stashahada ya Ualimu kutoka Chuo cha Ualimu Morogoro (2005 hadi 2007), na kuhitimu Shahada ya Ualimu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) kati ya mwaka 2007 hadi 2010.Dkt. Biteko aliendelea na elimu ya juu na kuhitimu Shahada ya Uzamili (Masters) kati ya mwaka 2011 hadi 2013.Safari ya Kisiasa Uwezo wake wa kiuongozi ulianza kung’aa mapema kupitia nafasi mbalimbali ndani ya chama, lakini mwaka 2015 aliandika historia kwa kushinda kiti cha ubunge wa Bukombe kwa tiketi ya CCM, akimshinda mgombea wa CHADEMA.

 Alichaguliwa tena kwa awamu ya pili mwaka 2020, akiendeleza kasi ya maendeleo katika jimbo lake.Uongozi wake ulianza kung’ara alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Madini mwaka 2017, na mwaka 2019 akateuliwa kuwa Waziri kamili wa Madini katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Agosti 30, 2023, Dkt. Biteko alipandishwa ngazi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa Naibu Waziri Mkuu (mratibu wa shughuli za Serikali) pamoja na Waziri wa Nishati, nafasi anayoshikilia hadi sasa.Kauli Maarufu na Wito kwa WananchiAkiamini katika uongozi unaotokana na ridhaa ya wananchi, Dkt. Biteko aliwahi kusema, “Uongozi unapewa na watu, sio mzazi wako.”Kwa msingi huo, wananchi wa Bukombe wanaalikwa tena kumpigia kura Dkt. Doto Biteko ifikapo Oktoba 29, 2025 kwa maendeleo zaidi ya jimbo.Maoni ya Wananchi kwa nyakati tofauti Juma Mahona, mkazi wa Ushirombo, amesema, “Hakika Doto ni mtu mzuri, anastahili kuchaguliwa tena.

Licha ya kuongezewa majukumu na Rais, bado ameendelea kutuletea maendeleo,”alisema Juma. 

Sarah Samson aliongeza kwa kusema, “Oktoba 29, 2025 tunasubiri kwa hamu kutiki. Tunampenda, anatuwakilisha vyema. Hakika wanaBukombe tunajivunia kuwa na Doto,” alisema Sarah. 

 
 

Comments