Leo, walimu Wilaya ya Bukombe mkoani Geita inaungana na dunia kuadhimisha Siku ya Mwalimu Duniani. Maadhimisho haya yanafanyika uwanja wa Ushirombo Sekindari Oktoba 3,2025 ikiwa mara ya sita mfululizo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2019.Tangu mwaka huo, Bukombe imekuwa ikiadhimisha siku hii muhimu kwa heshima ya walimu miaka ya maadhimisho ikiwa ni 2019, 2021, 2022, 2023, 2024, na sasa 2025.
Maadhimisho ya mwaka huu yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo mgombea ubunge wa Jimbo la Bukombe na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Doto Biteko.
Mgeni rasmi katika tukio hili muhimu ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Kassim.
Akizungumza kuhusu maandalizi, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Ramadhan Ng'oi, amesema kuwa walimu kutoka kata zote 17 za Wilaya ya Bukombe wamejitokeza kwa wingi kusherehekea siku yao wakiwemo wasani mbalimbali.
Ameeleza kuwa sherehe zinaendelea vizuri, zikiwa na lengo la kuwapa walimu nafasi ya kufurahi, kusherehekea mafanikio yao, na kuimarisha mshikamano.
Comments
Sr Vedastina Sottery
ReplyDelete
ReplyDeleteMungu...mwema ameniwezesha kuwepo siku ya leo hakika imeandaliwa...kwa ufanisi mkubwa..wenye fundisho.Acha mwalimu airway mwalimu.Nawaombea neema tele..Asante sana My.Dr Dotto..Borneo...
Ama kweli..Bukombe...siyo mchezo...kuna mambo makubwa hapa....Asante...waandaaji....Biteko hoyeeee Mwalimu day.Bukombe
ReplyDelete