DKT. SAMIA AAHIDI MIRADI MIPYA YA MAENDELEO WILAYANI BUKOMBE


Na, Ernest Magashi

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuendelea kuwekeza katika miradi ya maendeleo wilayani Bukombe, mkoani Geita, baada ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.Akizungumza katika mkutano wa kampeni zake, Dkt. Samia alisema kuwa Serikali itaongeza bajeti kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa wilaya hiyo, pamoja na kutoa ruzuku ya chanjo kwa mifugo, kujenga na kukarabati majosho, minada na machinjio."Tutainua sekta hizi kwa sababu Bukombe kuna wafugaji wafuge ng’ombe bora wa maziwa. Tutajenga viwanda vya kuchakata maziwa ili wafugaji wauze bidhaa zao na kukuza uchumi wao,” alisema Dkt. Samia.Ameongeza kuwa maendeleo ya mtu hayakamiliki bila huduma muhimu kama afya bora, elimu, maji safi na sasa serikali imeongeza sekta ya nne muhimu umeme. Alisisitiza kuwa kwa miaka mitano iliyopita, serikali yake imefanya kazi kubwa kupeleka huduma hizo, na baada ya uchaguzi, ataendelea kuziboresha.Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, ambaye pia ni mgombea ubunge wa Jimbo la Bukombe kwa tiketi ya CCM, alieleza kwa kina utekelezaji wa miradi hiyo akimpongeza Rais Samia kwa upendo wake kwa wananchi wa Bukombe.

Dkt. Biteko watu wema wa a Bukombe Mama Samia ametufanyia makubwa Bukombe.Akiomba kura kwenye mkutano huo, Dkt. Biteko alisema kuwa serikali ya Rais Samia imeleta mageuzi makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika historia ya Bukombe."Katika sekta ya kilimo tumepata ruzuku ya mbolea, pembejeo, na vituo viwili vya zana za kilimo vitajengwa  kimoja kata ya Namonge na kingine Bugelenga ili wakulima waachane na jembe la mkono," alisema.Aliongeza kuwa wilaya hiyo ilikuwa na shule moja tu ya kidato cha tano na sita, lakini sasa kuna shule tano, na kwa mara ya kwanza tangu Uhuru, wilaya hiyo inajengewa chuo cha ufunzi stadi (VETA) cha hadhi ya kitaifa.

"Chuo cha VETA kinachojengwa Bukombe kinahadhi ya kitaifa pia chuo cha Arusha kimeanzisha tawi hapa Bukombe. Usajili wa wanafunzi karibu unaanza, sasa watu wetu wanatembea kifua mbele," aliongeza Dkt. Biteko kwa furaha.Maji, Ofisi za Serikali, Barabara na Michezo Dkt. Biteko akizungumzia upatikanaji wa maji, alisema kuwa awali upatikanaji ulikuwa asilimia 25 lakini sasa umeongezeka hadi asilimia 65 kutokana na juhudi za serikali ya Dkt. Samia. Pia kuna zaidi ya miradi 22 ya inayoendelea.

"Mama Samia umetuletea mtambo wa kuchoronga maji hapa Bukombe, sasa tukihitaji maji, tunachimba na kuyapata kwa wakati," alisema huku akishukru Dkt. Biteko.Aliongeza kuwa tangu kuanzishwa kwa wilaya ya Bukombe mwaka 1996, haikuwa na jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya, bali ilitumika ofisi ya Tarafa. Hata hivyo, sasa jengo jipya la kisasa linaendelea kujengwa.

"Umesema tupige chini jengo la zamani, leo inajengwa ghorofa. Soko la zamani la miaka ya 90 pia unalibomoa tujenge jipya. Uwanja wa mpira wenye taa unajengwa ili michezo ichezwe usiku na mchana," alisema.Aidha, mtandao wa barabara umeongezeka kutoka kilomita 256 hadi kufikia kilomita 1,400, na barabara ya lami Ushiribo kwenda Katoro unaendelea kutekelezwa kwa kiwango cha lami."Mama Samia umetenda makubwa. Hatuna cha kukulipa bali kukuahidi kura nyingi Oktoba 29, 2025," alihitimisha Dkt. Biteko.Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Nicholaus Kasendamila, alisema kuwa chama kimejipanga kuhakikisha kuwa wanashinda kwa kishindo.

"Viongozi wote wa chama tumetawanyika kuomba kura za udiwani, ubunge na Urais. Lakini sisi hatuombi kura nyingi, tunaomba kura zote kwa Dkt. Samia, wabunge na madiwani wa CCM," alisema kwa msisitizo.

 

Comments