DKT. SAMIA AAHIDI KUIMARISHA SEKTA YA MADINI KWA MANUFAA YA WACHIMBAJI NCHINI


Na, Irene Makopudo

Katika mwendelezo wa kampeni za uchaguzi mkuu, viongozi mbalimbali wanaendelea kumimiinika kwenye mikutano ya hadhara  kumu unga mkono mgombea  Urais wa chama cha mapindunzi (CCM),Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

 Akizungumza na wananchi wa wilaya ya Bukombe mkoani Geita leo amesisitiza dhamira ya serikali  kuboresha sekta ya madini ili iwe na manufaa  zaidi  kwa wananchi na taifa kwa ujumla ,amesema serikali itaendelea  kuweka mazingira rafiki kwa wachimbaji wadogo wakiwemo wafanya biashara  wa madini ,ili kuongeza  uzalishaji  na mapato.Aidha, ameeleza kuwa uboreshaji wa miundombinu ya barabara za ushirombona katoro ni kipaumbele kwa lengo la kurahisisha  usafiri wa watu na bidhaa hivyo kuchochea maendeleo  ya kiuchumi katika wilaya Bukombe.Vilevile amebainisha  mpango wakujenga  chuo cha ufundi katika eneo hilo ili kuongeza  fursa za mafunzo kwa vijana na kuwawezesha kupata ujuzi utakaowawezesha kujiajiri na kushiriki kikamilifu  katika ujenzi wa taifa.Kwaupande wake  Mh Dkt Doto Biteko ameeleza  kuwa naimani na mama Samia kutokana na utekelezaji wa miradi  mikubwa ya maendeleo katika jimbo la Bukombe ,maana lilikuwa nyuma kimaendeleo  na sasa maendeleo yanaonekana kwa wazi bila shaka yoyote,ikiwemo ujenzi wa miundombinu,upanuzi wa huduma za afya na elimu pamoja na kuimarisha uchumi wa wananchi wa kipato cha chini,uteuzi wake ni kielelezo cha uongozi wa hekima ,uwajibikaji na uthubutu.

Hata hivyo ndugu Anton Mavunde ambae ni Waziri wa madini ameeleza kuwa wachimbaji wadogo wadogo wa madini wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiweo ukosefu wa mitaji ya kutosha,teknolojia duni ya uchimbaji,ugumu wa kupata masoko ya uhakika kwa madini wanayoyapata,kuna haja ya serikali na wadau wa maendelao kuongeza uwekezaji katika mafunzo ya uchimbaji bora,upatikanaji wa mitambo ya kisasa  kwa mikopo nafuu.


Comments