DKT. BITEKO AZUNGUMZA NA MAWAKALA WA CCM BUKOMBE


Na, Ernest Magashi

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukombe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Doto Biteko, amezungumza na mawakala wa chama hicho wa jimbo hilo katika kikao cha maandalizi kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.Mkutano huo umefanyika Oktoba 23, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa CCM Wilaya ya Bukombe, mkoani Geita.Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Biteko aliwahimiza mawakala kufanya kazi kwa uadilifu, uaminifu na kwa kuzingatia kanuni na taratibu za chama, ili kuhakikisha ushindi wa kishindo kwa CCM katika uchaguzi huo.Baadhi ya mawakala waliohudhuria wamesema kupitia mkutano huo wamepata uelewa mpana kuhusu majukumu yao na namna bora ya kutekeleza kazi zao kwa manufaa ya chama.

Comments