Katika mwendelezo wa kampeni zake za ubunge, Dkt. Doto Biteko, ameendelea kuvutia maelfu ya wananchi katika mikutano mbalimbali ndani ya jimbo lake, amesisitiza kuwa dhamira yake kuu ni kuendeleza miradi ya maendeleo ,kuboresha huduma za jamii na kuendelea kusikiliza sauti za wananchi.
Amezungumza hayo na wananchi katika mkutano wa 23 wa kampeni kata ya Bukombe kijiji cha Ikaranga, ameeleza mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitano, ujenzi na ukarabati wa shule na zahanati, upatikanaji wa maji safi na salama, kuboresha barabara za mjini na vijiji.
"Tumekuja kuomba kura kwasababu tunayo kazi yakufanya kwaajili ya kijiji na kitongoji, tunayo kazi yakubadilisha hali na maisha ya watu kwa kuleta maendeleo kwenye maeneno haya, Ikaranga ninayo ijua mimi ya miaka kadha niliyo ijua mimi, Ikaranga ambayo tulikuwa tunachukua muda kubishana, Ikaranga ile imekwisha badilika,"alisema Dkt. Biteko.
Dkt. Biteko ameeleza mafanikio ambayo yamepatikana katika kipindi chote ndani ya miaka mitano, kuwa Ikaranga haikuwa na umeme, barabara, maji, lakini kwasasa kuna barabara, umeme, shule, na maji, amewasisitiza wananchi kwenda kupiga kura siku itakapo fika maana maendeleo hayaji bila kupiga kura wananchi wajitokeze kwa wingi siku hiyo ya Oktoba 29,2025.
Kwaupande wake mgombea udiwani kata ya Bukombe Rozalia Masokola aliwashukuru wananchi kwa kujitokeza kwenye mkutano huo na kuwataka kujitokeza Oktoba 29 mwaka huu kupiga kura kwa wingi ili maendeleo ya wepo katika kata hiyo lazima watu wajitokeze siku ya kupiga kura, maendeleo yetu ni kura yako.

Comments
Post a Comment