Mgombea ubunge Dkt Doto Biteko anaendelea na kusaka kura katika wilaya nzima Bukombe katika kata na vitongoji vyote vya Bukombe.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Bweda kata ya Namonge waomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura na watakapopiga kura hiyo maana yake ni kutimiza wajibu wao wa kidemokrasia ambao utawawezesha kutimiziwa mahitaji yao ya kijamii.
Dkt. Biteko Katika mkutano wakampeni akiomba kura za Rais Dkt. Samia na udiwani ameeleza utekelezaji wa Ilani ya chama cha mapindunzi katika miaka mitano iliyopita ambapo utekelezaji wake umekuwa mkubwa ,katika kata ya Namonge na vitongoji vyake.
"Nataka nianze kwa kuwashukuru kwa ushirikiano ambao mmetupatia katika miaka mitano iliyo pita kama viongozi wa wakilishiwenu tumeona raha kufanya kazi ya uwakilishi kwanini?, kwasababu hakuna jambo tumepungukiwa katika kata yenu hii ni kata kubwa kati ya kata 17 katika wilaya ya Bukombe, ni kata yenye watu wengi na hii ni kata moja wapo,"alisema Dkt. Biteko.Aliongeza kuwa wakati wa uchanguzi katika kipindi kilicho pita ukanda huo wa Namonge ulikuwa ni ngome ya upinza ,ambapo walifungiwa njia ya kupita lakini watu wa Namonge walisimama imara ile ngome ili vunjwa na upinza haukuwepo tena ,watu waliamini chama cha mapindunzi (CCM) na kushikamana kwa umoja ili kupata maendeleo.
"Nataka niwaambie kazi tumeifanya tena kwa nguvu zetu zote ili tubadilishe hali ya maisha tu, eneo ili miaka iliyopita gemu wakiishiwa hela porini anakuja kutafuta hela kwa wananchi,watu wakawa wanaishi kwa mashaka,watu wakawa wanakanguliwa mbao hadi kwenye uvungu wa vitanda vya watu ,hali ya maendeleo haikuwepo,barabara hazikuwepo, tukitaka kwenda Namonge makao makuu hakuna barabara,"alisema Dkt. Biteko.Sambamba na hayo ameeleza walimu ambao waliotokea kupangwa katika kata hiyo walilia kwa sababu kulikuwa ni shida, maji ,umeme ,barabara, hospitali ,kwa ujumla maisha yalikuwa ni mangumu ,maendeleo ambayo yamepatikana kwasasa ni kutoka kwa Mama Dkt. Samia, barabara zote zitatengenezwa ili watu waweze kusafiri kwa urahisi bila usumbufu tena.
Kwaupande wake mgombea udiwani kata ya Namonge Mlalu Bundara ,aliwapongeza wananchi na kuwashukuru kwa dhati na kuwaomba wajitokeze siku ya Kupiga kura Oktoba 29 za Rais Samia ,Dkt. Biteko kwa wingi ili maendeleo yaendelee katika kata yao ya Namonge.
Comments
Post a Comment