Mgombea umbunge jimbo la Bukombe mkoani Geita, kwa tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Dkt. Doto Biteko aameahudi neema kwa vijana wa hamasa wilayani humo. Dkt. Biteko ameyasema hayo Oktoba 27,2025 kwenye mkutano wa hadhara wa kufunga kampeni zake uwanja wa CCM kata ya Igulwa.
Kampeni za uchaguzi katika wilaya ya Bukombe zimehitimishwa kwa hamasa kubwa zikiongozwa na Naibu Wazari Mkuu na Wazari wa Nishati,Dkt Doto Biteko, ambaye ni mgombea ubunge wa jimbo la Bukombe kupitia chama cha mapinduzi (CCM).
Katika mkutano huo wa kufunga kampeni uliofanyika katika viwanja vya kata ya Igulwa ambapo mamia ya wananchi wamejitokeza kumsikiliza ,amewataka wananchi kuchukua nafasi yao kwa vitendo na sio kwa maneno kwenda kupiga kura.
Akizungumza katika hotuba yake wakati wote ameonesha nia yake ilivyokuwa sehemu ya kampeni zake nikujenga uchumi wenye utendaji,usambazaji wa umeme na gesi,na kuinua maisha ya wananchi wa Bukombe ,alisisitiza kuwa siyo tu kumaliza kampeni bali kuahidi kuendelea na jitihada za kuthibitisha ahadi zake mbele ya wananchi.
"Niwashukuru sana vijana wetu wa hamasa wilaya ya Bukombe, hawa vijana hakuna siku utawaona wamechoka,kila siku ni kama wananguvu mpya vijana wa Bukombe Mimi siwadai ninyi mnanidai mimi na nikisema hivyo mnaelewa nataka niwahakikishie nitafanya kila ninaloweza lililo ndani ya uwezo wetu ,vijana hawa wasikomee kuwa vijana kwenye mikutano ya kampeni lazima maisha yao tushughulike nayo lazima tuwe na mpango wa vijana hao ,chama hiki kinapiganiwa na wazee,wanawake, na vijana hata watoto,"alisema Dkt. Biteko.
Aliongeza kuwa kila wakati anapoana wananchi wanajitokeza katika mikutano ,na hata anapoona wananchi wamechagamka, hata kunapokuwa imeitishwa mikutano hiyo huwa ni deni kwake maana heshima hiyo imekuwa kama vile hakustahili kupewa ,aliwashukuru wananchi pamoja na viongozi wote walioshirikiana katika kipindi chote cha kampeni.
" Tuendelee kupendana miongoni mwetu, tupendane jamani Tanzania hii ni yetu, upendo unazaa amani, nataka nieleze amani kwa mapana yake, tumehubiliwa sana amani nataka niwaambie, makundi matatu jinsi ngani tunahusika na kushikilia amani katika uchaguzi huu, kundi la kwanza ni vijana, kila mzee anaye zeeka anakabithi kijana, nchi hii ni ya kwenu, chama hiki ni chakwenu kishikilieni tunzeni amani na kujitokeza kupiga kura,"alisema Dkt. Biteko.
Sambamba na hayo, mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita Nicholas Kasendamila alianza kwa kuwashukuru wananchi kwa kushiriki katika kampeni kipindi chote cha kampeni hizo, na kusisitiza upendo ambapo upendo huzaa amani.

Comments
Post a Comment