WAZIRI MKUU MAJALIWA KUFUNGUA MAONYESHO YA MADINI GEITA

Na, Salum Maige

 Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa maenyesho ya 8 ya Kitaifa ya teknolojia ya Madini yanayofanyika mjini Geita ,mkoani Geita.

Mkuu wa mkoa wa Geita amesema Waziri mkuu atawasili jumatatu ya septemba 22 ,mwaka huu mjini Geita kisha kuwahutubia wananchi katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan vilivyopo mtaa wa Bombambili, Mansipaa ya Geita.

Hivyo, amewataka wananchi wa mkoa wa Geita kujitokeza kwa wingi katika ufunguzi huo ,pamoja na kupata fursa ya kutembelea maonyesho hayo kujionea bidhaa mbalimbali zikiwemo za madini na hifadhi za wanyama.

Aidha ,amesemna maonyeshi hayo yanashirikisha washiriki 1,200 kutoka ndani na nje ya nchi , idadi hiyo ni zaidi ya mara mbili ya washiriki 530 wa mwaka jana.

“Niwashihi wananchi maonyesho haya yameleta fursa kubwa kwa wafanyabiashara wa ndani na nje, na ikumbukwe kuwa mkoa wa Geita umekuwa unazarisha tani 56,000 katika kipindi cha miaka mine hivyo ni mkoa unaongoza kwa uzalishaji wa madini ya dhahabu” amesema Shigela.

Afisa Madini Mkazi mkoa wa kimadini wa Geita, Samweli Shoo amesema maonyesho yamewezesha wachimbaji wadogo wa mkoa wa Geita kukutana na wadau mbalimbali wa madini ambao hushiriki kuchimba kisasa.“Tumekuwa na mafanikio hasa msaada wa kiufundi ambao wamekuwa wakiwaletea teknolojia ya kiufundi kwa wachimbaji, maonyesho hayo yameleta uchenjuaji wa kisasa na kwamba mafanikio makubwa yamepatikana,” amesema Shoo.

Ameongeza kuwa wakati wachimbaji wadogo wa madini wanatumia zebaki katika uchakataji walikuwa wanazalisha Kilo 2000 za madini ya dhahabu ,lakini kutokana na kuongezeka kwa teknolojia ya CIP uzalishaji umefikia kilo 4000 kwa mwaka.

Mfanyabiashara wa madini Leonard Bugomola amesema maonyesho hayo yamesaidia wachimbaji walio wengi kuhama kwenye matumizi ya zebaki iliyokuwa ikiathiri hata watu wengine ambao hawajishughulishi na madini kupitia maji na vumbi.“Naomba watu wajitokeze kuja kwenye maonyesho haya wajifunze vitu vingi, Pia waje wananchi wawekeze Geita kujenga nyumba za kulala wageni kwani watu ni wengi wanaingia Geita, niwaombe tu wafanyabiashara waje wawekeze Geita” amesema Bugomnola.

Maonyesho hayo yanafanyika katika Uwanja wa Dkt.Samia Suluhu Hassani Bombambili mjini Geita yakiwa na Kauli Mbiu,”UKUAJI WA SEKTA YA MADINI NA MATOKEO YA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA SAHIHI NA UONGOZI BORA,SHIRIKI UCHAGUZI MKUU”.


 

Comments