WARATIBU WA PJT-MMMAM GEITA WAPEWA MAELEKEZO NA SERIKALI


Na, Salum Maige

Waratibu wa programu jumuishi ya Taifa ya malezi, makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto(PJT-MMMAM)  waliopo kwenye halmashauri zote za mkoa wa Geita wameelekezwa na kusisitizwa kusimamia utekelezaji wa progarmu hiyo ili kufikia lengo la ukuaji timilifu kwa watoto.Maelekezo hayo yametolewa na Dkt. Stephen Mwaisobwa aliyemwakilisha mganga mkuu wa mkoa wa Geita Dkt. Omari Sukari kufunga kikao cha mapitio ya tathimini ya utekelezaji wa program hiyo kwa kipindi cha januari hadi juni 2024/2025.Dkt. Mwaisobwa amesema utekelezaji wa program hiyo uambatane na kuweka mipango kazi kutenga bajeti kwa ajili ya kuhakikisha lengo la serikali kuanzisha program hiyo linafikiwa kwa kutoa afya bora, lishe bora, ujifunzaji wa awali, malezi yenye mwitikio na ulinzi na usalama kwa mtoto.

“Wasimamizi wa makao ya watoto, vituo vya kulea watoto na wadau wote mnaohusika na ulinzi na usalama wa mtoto nanyi mnahitajika kuweka mipango kazi ya kusaidia utekelezaji wa program hii kwenye maeneo yenu ikiwa ni kuunganisha nguvu za kuhakikisha afua za malezi, makuzi na maendeleo ya watoto zinazingatiwa” alisema Dkt. Mwaisobwa.Aidha, ameyaelekeza mashirika yasiyo ya kiserikali yakiongozwa na shirika la NELICO ambalo linatekelezaji mradi wa mtoto kwanza kwenye mkoa wa Geita kuhakikisha wanaitisha vikao vya mashirika yasiyo ya kiserikali kukaa na kutenga bajeti ,kuweka mikakati ya namna ya kufanikisha mpango huo wa serikali.Awali, afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Geita Martha Kaloso program hiyo inalenga umri wa mwaka 0 hadi 8 ikiwa ni kukabiliana na changamoto zinazoonekana kuwa ni kikwazo cha hatua sahihi za ukuaji timilifu wa watoto kiwmili, kiakili na kijamii.Alisema, kwa mujibu wa wa tafti za kisayansi imeonyesha kuwa huo ndiyo umri nyeti wa kumtengeneza mtoto aliye bora au mtoto aliyedhaifu kimwili , kiakili na kijamii kwa kuwa katika umri huo ubongo hupokea kile kinachoingia nna mwili kujengwa kutokana na kile anachopatiwa.

Akisoma taarifa ya utekelezaji program hiyo mratibu wa mradi wa mtoto Kwanza mkoa wa Geita ,Sophia Njete kutoka shirika la NELICO lengo kuwepo kwa mradi huo ni kuwekeza moja kwa moja kwenye maendeleo ya watu ili kurahisisha upatikanaji wa matokeo chanya ya maendeleo ya awali ya mtoto.

“Ujio wa mpango huo ni kuhakikisha tunatoa huduma za malezi jumuishi yenye vipengele vitano, ambavyo ni afya bora kwa mtoto na mama/mlezi, lishe ya kutosha kuanzia ujauzito, malezi yenye mwitikio, fursa za ujifunzaji wa awali na ulinzi na usalama kwa mtoto” alisema Njete.

Pia, aliongeza kuwa hatua hiyo ya serikali na wadau ni kuhakikisha watoto wote nchini Tanzania wapo kwenye maendeleo sahihi wa kufikia ukuaji timilifu na kufikia lengo namba 3 na 4 la maendeleo endelevu SDGs kufikia 2030.

Kwa taarifa ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 ,mkoa wa Geita unakadiriwa kuwa na jumnla ya watu 2,977,608 ambapo wanaume 1,463,764 na wanawake ni 1, 513,844 kati ya watu hao watu 946,879 sawa na asilimia 31.8 ni watoto wa umri wa chini ya miaka mitano.


 

Comments