Na ,Irene Makopudo
Wananchi wajitokeza kwa wingi kumsikiliza Mgombea Ubunge Jimbo la Bukombe Mkoa wa Geita Dkt Doto Biteko kwenye mkutano wake wa kampeni katika kata ya Uyovu kwa kusikiliza sare.
Katika mkutano huo wa kampeni Dkt. Biteko ameahidi maendeleo katika kata ya Uyovu kwa kuifanya Uyovu kuwa ni kata yenye maendeleo ,ameahidi ujenzi wa stendi ya Malori na bodaboda ili kuepusha ajali ambazo huwa zinajitokeza mara kwa mara katika kata hiyo.
"Kata ya Uyovu ilikuwa haina maendeleo kabisa leo kuna sekondari nyingi na shule za msingi zimeongezeka tunataka tuongeze miundombinu tunataka tujenge hospitali, nataka niwaambie watu wa Uyovu mna neema ya kuzaa watoto, tumejenga shule maalum ipo hapa Uyovu na Ushirombo, na stendi ambayo tunajenga lazima iwe ya kisasa,"alisema Biteko.
Ameongeza kuwa Uyovu kuna mradi wa maji ambao unaendelea katika kata ya Uyovu, miaka mitano ijayo Uyovu itakuwa ya kisasa.
Vilevile amesema kuna fedha zimetengwa ili kuweza kusaidia vijana na wakinamama kwaajili ya kuwakopesha ili waweze kufanyia biashara ilikuleta maendeleo katika kata hiyo ya Uyovu ,katika kata hiyo itakuwa jicho la Dkt Biteko kuanzia Januari hadi Desemba.
Sambamba na hayo mgombe udiwani Matayo Kagoma aliwapongeza wananchi kwa kufika kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni hizo jinsi wameweza kufika kwenye mkutano ,aliahidi kuleta maendeleo.
Alisema katika kata hiyo japo maendeleo yapo lakini pia bado yanahitajika ili kukambiliana idadi ya watoto ambao wanaongezeka kwahiyo agenda ya kumchangua Dkt. Biteko ni muhimu kwa maendeleo.

Comments
Post a Comment