WALIMU BUKOMBE KUSHEREKEA SIKU YAO OKTOBA 3,2025


Na, Ernest Magashi

Maadhimisho ya siku ya Mwalimu duniani yatafanyika wilayani Bukombe Oktoba 3, 2025 ambapo mgeni rasmi ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.

Maadhimisho hayo ambayo hufanyika kila mwaka wilayani humo yataambatana na sherehe na matukio mbalimbali ya kutambua na kupongeza kazi za walimu.

Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Walimu wetu, fahari yetu."

Mratibu wa maadhimisho hayo, Mwalimu Abdulmajid Yusuph ametaja wadhamini kuwa Chama cha Walimu wilaya ya Bukombe, benki ya CRDB, Radio Jembe ni Jembe fm, pamoja na wadhamini wengine.

Aidha, walimu wote kutoka shule za serikali na binafsi wanatarajiwa kuhudhuria tukio hilo kubalishana uzoefu na kupongezana ambapo tuzo mbalimbali hutolewa na wadau wa maendeleo.

Maadhimisho yatafanyika kiwilaya viwanja vya shule ya Sekondari Ushirombo ambapo Uongozi wa CWT wilaya ya Bukombe unasema mwaka huu itakuwa Kubwa Kuliko miaka yote huku wakitoa ukaribisho kwa Watu wema wa Bukombe wa Kusema Na Kutenda kufika kwa wingi ili kusherekea pamoja na kujifunza.

Comments