WAJA: KUKAMILISHA MIRADI ILIYOACHWA NA MTANGULIZI WAKE

Na, Salum Maige

Mgombea ubunge wa jimbo la Geita Mjini Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Mhandisi Chacha Wambura amesema atahahakikisha miradi iliyokwama kipindi cha mtangulizi wake inakamilika ikiwemo ujenzi wa Stendi ya kisasa, na mradi mku wa maji kutoka Ziwa Victoria.

Akizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya kampeni amesema, Mtangulizi wake Costantine Kanyasu alifanya mambo mengi katika kipindi chake cha miaka 10 ,hivyo naye akipewa ridhaa na wananchi kuwa mwakilishi wao kwenye mhimili wa bunge ataanzia alipoishia mwenzake na kuendeleza miradi iliyopo na mingine mipya.Mhandisi Wambura alimaarufu Waja anaendelea na kampeni zake za kujinadi kwa wananchi huku akija na kauli Mbiu  isemayo “Geita Mpya” ,Kazi na Matokeo” akimaanisha anaenda kubadilisha jimbo la Geita mjini kuna na kasi ya Maendeleo ikiwemo miradi iliyoachwa na mtangulizi wake.

Moja ya miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa mradi wa stendi mpya ya kisasa ya Manispaa ya Geita mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria unaotekelezwa kwa thamani ya bilioni 128 ambao utakuwa kutatua maji kwa wakazi wa Mansipaa ya Geita.Amesema anafahamu wananchi wa Mji wa Geita wanahitaji maji ambayo yamekuwa ya mgawo kila kukicha ,hivyo jambo ambalo ataenda kulisimamia ni utekelezaji wa mradi huo ambao utanufaisha wananchi wa jimbo zima la Geita na kwenda kufuta tatizo la mgawo wa maji.

Aidha, katika kampeni zake jambo lingine ambalo anadai linamuumiza kichwa ni barabara ya kutoka Kahama hadi Geita ambayo inatakiwa kujengwa kwa kiwango cha Lami ili kuondoa usumbufu wa kuzunguka Bwanga ,Ushirombo kwa safari za kwenda Dar es Salaam na mikoa jirani.Kubwa kuliko, Mhandisi Wambura amesema, katika ilani ya uchaguzi ya mwaka 2025 /2030 inaonyesha kuwa Geita kunaenda kujengwa chuo kikuu ambacho kitasaidia wananchi kuwepo kwa mzunguko wa fedha.

“Hili nitaenda kulisimamia kwa sababu lipo kwenye ilani, tukipata chuo kikuu hapa mzunguko wa hela utakuwa mkubwa, tukiwa na wanafunzi 10,000 au 50,000 hawa watahitaji kupanga, watahitaji chakula, watahitaji kusuka na kunyoa, kwa hiyo mzunguko wa hela utaongezeka katika mji wa Geita” amesema Mhandisi Wambura.Mgombea huyo mbali na miradi hiyo amesema, ataenda kusimamia suala la elimu, Afya na miundombinu ya barabara kwa kuhakikisha mahitaji yote ya muhimu katika sekta ya hizo yanapatikana ikiwa ni pamnoja kuongeza miundombinu ya vyumba vya madarasa, vituo vya Afya na barabara za lami zinaongezeka kwenye mji wa Geita.


 

Comments