WAJA AMWASHIA TAA NYEKUNDI MKANDARASI WA KILOMITA 17 ZA LAMI


Na, Salum Maige

Mgombea ubunge jimbo la Geita Mjini kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Mhandisi Chacha Wambura amesema endapo atapewa ridhaa na wananchi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 atahakikisha mkanndarasi wa barabara za lami kilomita 17  anazikamilisnha kwa wakati ili kuondoa kero kwa wananchi.

Mhandisi Wambura ametoa kauli hiyo kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika Mtaa wa Shilabela kata ya Buhalahala.Amesema amegundua kuwa mkandarasi wa barabara hizo zinazopita kwenye kata za Mtakuja, Kalanngalala, Buhalahala, Nyankumbu na Bombambili anafanya kazi kwa kusuasua hali inayoleta usumbufu kwa wananchi.

“Hizi barabara zina muda mrefu mkandarasi anahangaika nazo ,nimegundua huyu mkandarasi ni mzembe ,barabara hizi kwa heshima ya mama yetu Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan lazima nikasimamie zikamilike kwani zimegeuka kama usumbufu kwa watu” amesema Wambura.

Ameongeza pia kwa kuwa serikali imeupandisha mji wa Geita na kuupa hadhi ya Manispaa unahitaji barabara nyingi za lami na mitalo ambayo itaruhusu maji kupita.

“Niwaambia wananchi Manispaa yetu inahitaji barabara nyingi za lami ,niwaambie inaenda kung’aa kwa lami, taa za barabarani, zipo barabara ambazo tutazijenga kwa mapato yanayotoka kwenye mgodi wetu wa GGM” amesema Wambura.Aidha, aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo la Geita mjini 2015 hadi 2025 Costantine Kanyasu alihudhuria mkutano huo na kumuombnea kura mgombea huyo huku akiwataka wapambe wake kumuunga mkono Wambura ili kuhakikisha anashinda katika uchaguzi huo.

“Hata mimi wakati naingia wana CCM hawakuamini kama nitafanya, lakini nilifanya na nikatambulika kwa wananchi, hata huyu rafiki yangu Waja(Chacha Wambura) atafanya hivyo tuwe na imani naye, na maendeleo hayawezi kuletwa na mtu mwingine tofauti na wa CCM” alisema Kanyasu.

Awali mgeni rasmi wa mkutano huo ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa wanawake UWT Taifa Mary Chatanda amewataka wananchi kuitunza amani ya taifa katika kipindi hiki cha uchaguzi kwani amani hiyo imesimamiwa kikamilifu na Rais Dkt Samia aliyepokea uongozi kwenye kipindi kigumu cha msiba wa Dkt. JohN Magufuli.Akimuomnbea kura mgombea ubunge Wambura, amesema pamoja na wapinzani kuweka mpira kwapani wananchi wajitokeze kwenda kupiga kura za NDIYO mgombea huyo na kumpigia Rais Dkt. Samia pamnoja na madiwani wa CCM.


 

Comments