STAMICO KUWAINUA WACHIMAJI WADOGO NCHINI

 

Na, Salum Maige 

Mkurugenzi wa shirika la madini Taifa STAMICO Venance Mwase amesema shirika hilo litaendelea kuunga mkono juhudi za wachimbaji wadogo wa madini hapa nchini kwa kutoa vifaa vya kisasa ili kwendana na teknolojia itayorahisisha shughuli za uchimbaji.

Amesema, serikali kupitis shirika hilo imewawezesha wachimbaji wadogo wa madini mitambo 15 kwa ajili kurahisisha shughuli na kuwaondoa kwenye uchimbaji wa zana duni zinazotumia muda mrefu kufikia uzalishaji.Mwase amesema hayo kwenye maonyesho ya kitaifa ya 8 ya teknolojia ya madini yanayofanyika katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan vilivyopo mtaa wa Bombambili manispaa ya Geita, mkoani Geita.

“Sisi kama shirika la madini, tunao wajibu wa kuhakikisha wachimbaji wadogo wanaondokana na uchimbaji wa kutumia zana duni, kupitia maonyesho haya wachimbaji wananufaika na upatikanaji wa elimu ya matumizi ya teknolojia ya kisasa,” amesema Mwase.

Katibu wa chama cha wachimbaji wa madini wanawake(TAWOMA)Salma Ernest amesema Serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanikisha kutoa leseni 17 pamoja na mitambo ya itakayowawezeha wananwake katika shughuli za uchimbaji.“Tunaipongeza sana serikali ya awamu ya sita chini ya jemedali Rais wetu Dkt. Samia kwa kutuwezesha vifaa vya kisasa kwa kweli sisi kama wachimbaji wadogo wanawake tumepiga hatua kubwa kupitia uwezeshwaji wa serikali ambayo imetupatia mitambo ya kisasa kabisa” amesema Salma.

Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela amesema maonyesho ya mwaka huu yamehusisha washiriki zaidi ya 1200 kutoka ndani na nje ya nchi kutoka washiriki 530 walioshiriki kwenye maonyesho ya mwaka jana.Amesema maonyeho hayo yenye kauli mbiu inayosema ‘Ukuaji wa sekta ya madini ni matokeo ya matumizi ya teknolojia sahihi na uongozi bora, shiriki uchaguzi mkuu 2025’ yameanza septemba 18 na yatatamatika septemba 28,mwaka huu.

Afisa madini mkazi mkoa wa Geita Samwel Shoo amesema uwepo wa maonyesho hayo imesaidia wachimbaji wadogo kukutana na wadau wenye mitambo ya kisasa na kuingia nao mikataba ikiwa ni hatua ya kuondokana na matumizi ya zana duni.

Amesema kipindi cha nyuma wachimbaji wa madini walikuwa wakizalisha kilo 2000 za dhahabu katika mkoa wa Geita lakini baada ya kuanza kutumia vifaa vya kisasa uzalishaji umeongezeka na kufikia kilo 4000 za dhahabu kwa mwaka.

 

Comments