Mgombe wa ubunge katika jimbo la Bukombe Dkt Doto Biteko ameendelea na kusaka kura za Ubunge na za Rais Dkt. Samia na madiwani mapema leo amefika katika kata ya Runzewe mashariki, na kunadi sera za CCM na Ilani ya chama hicho huku akieleza mafanikio ya miaka kumi katika ubunge wake na kuwaomba kura wakazi wa kata hiyo.
Katika mkutano huo wa kampeni amewataka madiwani kuende kusaka kura bila kuchoka kura za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt Doto Biteko ,bila kusahau kura za madiwani katika kata zote jimbo la Bukombe.
"Miaka mitano inayokuja tunataka tulete maendeleo na siyo maneno naahidi kutengeneza barabara, uchanguzi huu unamahusiano kwenu na maendeleo hakuna maendeleo yatatokea kama hamtapiga kura mjitokeze kupiga kura ili maendeleo yaje kwenu, na hakuna chochote utakacho mpatia mtoto wako kama siyo elimu kwahiyo tusomeshe watoto wetu ili waje kuwa viongozi wanzuri,"alisema Dkt. Biteko.
Aliongeza kuwa maendeleo hayajitu lazima watoto wasome alisisitiza kwa wazazi na walezi kusomesha watoto ,maana bila elimu hakuna kitu ambacho kinaweza kufanyika katika maendeleo ya kata hiyo,ili maendeleo yawepo lazima kupiga kura kwa wingi na kusomesha.
Sambamba na hayo mgombe udiwani wa kata ya Runzewe Mashariki Mary Nchiba alieleza maendeleo ambayo yamefanyika katika kipindi chote ambapo yeye alikuwa diwani.
Nchiba alizitaja sekta zote ambazo zimeweza kufikiwa na ukarabati wa zahanati na shule za sekondari na msingi pamoja na sekta ya miundombinu na sekta ya maji .

Comments
Post a Comment