Mwenyekiti wa chama cha mapindunzi CCM Wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita Matondo Kihanda amenzindua kampeni za udiwani CCM kata ya Katente.
Katika uzinduzi huo mwenyekiti amemukabidhi mgombea udiwani Ilani ya CCM humu akiwaomba Wananchi Oktoba 29,2025 kupiga kura nyingi.
Kihanda aliwashukuru wakazi wa kata ya katente kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo kusikiliza sera za Mgombea.
Alitaja jitihada za miradi ya maendeleo zilizofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan miaka mitano ambayo imepita na kuwataka wakazi wa katente wampigie kura tena kwa maendeleo mengine ambayo atayafanya.
Mgombea udiwani kata ya Katente Tabu Ng'hwani ameeleza jitihada ambazo zimefanywa na Mbunge Dkt. Biteko na Rais Dkt. Samia ni kubwa ya kuleta maendeleo kata hiyo ya katente.
Ng'hwani akiomba kura kwa wananchi amesema pamoja na maendeleo yote katika jimbo la Bukombe, Serikali ya Rais Dkt. Samia katika kuwaletea maendeleo wananchi imetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Maabara na zahanati, shule za msingi na sekondari na miradi ya kimkakati inaendele.
Mkazi wa Katente Nyazara Bapala amesema ataendelea kumuunga mkono mgombea udiwani Ng'hwani, Ubunge Dkt. Biteko na Dkt. Samia kwa kazi kubwa nzuri waliyoifanya ya kuleta miradi nakuisimamia haliambayo inawafanya wananchi kuwanahali nzuri ya kiuchimi.

Comments
Post a Comment