Mwenyekiti wa chama cha Mapindunzi CCM Wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita Ndugu Matondo Lutonja amenzindua kapen za udiwanui kata ya Igulwa huku akieleza ilani ya chama cha mapindunzi na miradi ambayo iliyotekelezwa na Mwenyekiti wa chama cha mapindunzi Taifa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hasani.
Akizungumza na wakazi wa kata ya Igulwa ameeleza Ilani hiyo na kumkabizi Ilani ya chama cha mapinduzi diwani Richard Mabenga na kumuombea kura kwa wakazi wa kata hiyo,huku akimpongeza kwa kazi ambazo amefanya za maendeleo kwa jamii katika kata ya Igulwa.
Mgombea udiwani kata ya Igulwa Richard Mabenga amefafanua utelezaji wa maendeleo katika ngazi ya kata ya Igulwa huku akimpongeza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko na mgombea ubunge Jimbo la Bukombe kwa maendeleo ambayo ameyafanya katika jimbo lake huku akitaja miradi mikubwa ya kimikakati inayotekelezwa katika kata ya Igulwa.
Sanjali na hayo ameweza kuitambanaisha katika hadhala hiyo, utekelezaji wa sekta ya miundombinu ya barabara za kata ya Igulwa sekta ya afya, ongezeko la vituo vya afya na uboreshaji wa vituo hivyo ,sekta ya maji napo wamefanikiwa kuwa na mradi wa maji safi na salama katika kata hiyo ,na katika sekta ya nishati sasa wakazi wa Igulwa mambo ni safi mno.
Amesema vilevile kata ya Igulwa katika sekta ya elimu haikubaki nyuma imetekeleza mradi wa shule pamoja na vyuo na katika sekta ya biashara haikuwa mbali imeweza kutekeleza mradi mkubwa wa kimkakati kwa kuanzisha unjezi wa mradi wa soko kubwa la kisasa, stendi ya mabasi na uwanja mkubwa wa mpira wa kisasa.

Comments
Post a Comment