MGOMBEA UBUNGE GEITA MJINI ATAJA VIPAUMBELE VITANO

 

Na, Salum Maige

Mgombea ubunge jimbo la Geita mjini wa chama cha nmapinduzi CCM Mhandisi Chacha Wambura ametaja vipaumbele vitano atakavyovifanyia kazi baada ya kupewa ridhaa na wananchi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu utakaofanyika oktoba 29.

Mhandisi Wambura ametaja vipaumbele hivyo kuwa ni elimu, Afya ,Miundombinu ya barabara, elimu ya ujasiliamali, na ajira kupitia sekta ya madini.

Mgombea huyo ametaja vipaumbele hivyo alipotembelea vijiwe vya Kahawa vilivyopo mjini Geita kikiwemo Kijiwe maarufu cha Mlumba, Kwa Mgosi, Nyankumbu na Soko la Mwatulole.Akifafanua utekelezaji wa vipaumbele hivyo Mhandisi Wambura alimaarufu Waja amesema katika sekta ya elimu atahakikisha anaboresha mazingira ya shule ikiwemo miundombinu madarasa ,mazingira ya walimu ili watoto waweze kusoma kwenye mazingira rafiki ambayo yatawasaidia kupata elimu bora.

Mimi kwenye elimu nina uzoefu kwa sababu na mimi nina miliki shule, hivyo uzoefu nilionao ni mkubwa ,nitahakikisha walau shule zetu za msingi na sekondari zinakuwa na mazingira rafiki ya kujifunzia” alisema Wambura.Kuhusu Afya ,amesema pamoja na serikali kujitahidi kujenga Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali ya Rufaa katika Manispaa ya Geita, atahakikisha kunakuwa na vifaa vya kutosha vitakavyowezesha wananchi kupata huduma bora na kwa haraka zaidi.

Ili ufanye kazi vizuri na uchumi upande lazima kuwa na Afya bora, huwezi kufanyakazi ukiwa unaumwa, hivyo ni Afya kwanza, nitahakikisha huduma za Afya zitakazokuwa zinatolewa ziwe bora zaidi sambamba na kuboresha miundominu yake

Kwa upande wa miundombinu ya barabara, amesema endapo atapewa ridhaa ya kuwa mwakilishi katika muhimili wa Bunge atahakikisha miundombinu ya barabara inapitika kipindi chote iwe kiangazi au masika kwa kuziunganisha kata zote na mitandao ya barabara zikiwemo za molamu na lami.

Akizungumzia suala la ajira kwa vijana kwenye sekta ya madini, amesema atazungumza na uongozi wa mgodi wa Geita GGML kutoa kipaumbele kwa vijana wa Geita zinapotokea ajira badala ya kuajiri watu ambao si wazawa wa Geita.

Mimi ni Mjanja ninafahamiana na Mgodi wetu huu ,nitafanya mazungumzo nao ili zinapotokea ajira tuanze na watu wa Geita ,tutatengeneza mfumo wa utambuzi(Data base) wa vijana waliomnaliza Kidato cha nne ili tuwape kipaumbele”amesema Waja.

Aidha, amesema ataiomba serikali pamoja na mgodi huo walau kuachia baadhi ya maeneo yake ili kuyatoa kwa wachimbaji wadogo hasa vijana waweze kujiajili na kujipatia kipato cha familia na taifa.

Kwenye elimu ya Ujasiriamali amesema, kwa kuwa anauzoefu wa biashara ataweka mfumo wa kutoa elimu kwa vijana ya ujasiriamali na elimu ya mikopo inayotolewa na serikali ili kuwawezesha mtaji ambao utakuwa biashara zao.

Kuna mikopo inatolewa na serikali lakini nyinyi wananchi hamna elimu ya mikopo hiyo, haya unakopa sasa halafu huna elimu na huna elimu ya ujasiriamali ,ukichukua hela matokeo yake unashindwa uifanyie kazi gani ,unaila inaisha na unashindwa kurejesha, sasa mimi nitahakikisha tunatoa elimu kwanza. 

 “Akizungumzia kuhusu Ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2025 hadi 2030 kwa mkoa wa Geita kunaenda kujenga chuo kikuu na soko kubwa la machinga na kwamba kutekelezwa kwa miradi hiyo itachochea uchumi wa Geita na kuleta mzunguko mkubwa wa fedha.Mbali na vipaumbele hivyo, amesema baada ya kushinda katika uchaguzi huo atafuatilia ujenzi wa choo kwenye soko la Mwatulole, na utekelezaji wa ahadi ya serikali ya kuijenga barabaraba ya lami kutoka Geita hadi Kahama ili kuondoa usumbufu wa kuzunguka kupitia Bwanga, Runzewe na Ushirombo wakati wa kwenda mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam ,Morogoro na Arusha.

Mhandisi wa Wambura anatarajia kuzindua Kampeni zake Septemba 17 ,na hivyo katika uzinduzi huo atataja mambo atayoanza nayo ndani ya siku 100 nza kwanza.

Mwenyekiti wa kamati ya kampeni ya Mgombea huyo, ambaye ni mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM Robert Nyamaigoro amewataka wanachi siku ya kupiga kura kujitokeza kwa wingi kwenda kushiriki uchaguzi hapo oktoba 29 ,na kuchagua wagombea wa CCM.

Mwarobaini wa kero zenu ni kujitokea kupiga kura, unapoenda kupiga kura unakuwa na haki ya kuhoji kwa nini kuna kero hii aidha ya barabara, maji, umeme, elimu au sekta ya Afya, na niwaambie CCM ndiyo inawagombea wazuri wenye uwezo wa kutatua changamoto hizo” amesema Nyamaigoro.

Katibu wa itikadi uenezi na mafunzo Andrew Mnunke amesema tangu chama cha mapinduzi CCM kushike dola nchi imekuwa na amani na kwenye amani lazima kuwe na maendeleo hivyo akasisitiza kuhakikisha wananchi wanatunza tunu ya amani hasa kwenye kipindi hiki cha kampeni hadi uchaguzi.

 

Comments