MAJALIWA, AFUNGUA MAONYESHO, AVUTIWA NA BANDA LA STAMICO

Na, Salum Maige

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa ameziagiza Taasisi za serikali na binafisi zinazojishughulisha katika sekta ya madini kuongeza thamani na kuhakikisha uchimbaji wa madini unafanyika kwa usalama bila kutokea ajali.Majaliwa ametoa agizo hilo wakati akiwahutubia wananchi kwenye ufunguzi wa maonyesho ya 8 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita.Majaliwa ameagiza viongozi hao kuhakikisha usalama unakuwepo katika maeneo ya uchimbaji ,kuongeza thamani katika uchimbaji wa madini ,kusimamia mazingira ili kuongeza tija katika uzalishaji wa madini nchini.Aidha, amezitaka halmashauri zote mkoani Geita kukaa kwa pamoja kuweka mpango mkakati wa kuongeza ujenzi wa mabanda ya kudumu katika viwanja vya Dkt.Samia Suluhu Hassani Bombambili yakufanyia kila mwaka maonyesho hayo.“Viongozi wa serikali simamieni hilo, kwani ili kuongeza thamani ya maonyesho kuwa na hadhi ya kitaifa na kimataifa ,yanahitajika mabanda ya kisasa na ya kudumu, pia simamieni uhifadhi wa mazingira,” alisema Majaliwa.Kabla ya kufungua maonyesho hayo yaliyoanza septemba 18 mwaka huu Waziri mkuu alitembelea mabanda mbalimbali likiwemo banda la Shirika la madini la Taifa STAMICO kujionea Teknolojia ya kisasa katika uchimbaji wa madini.Akitoa ufafanuzi wa teknolojia hiyo Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO Deusdedith Magala amesema shirika hilo limekuwa likitoa msaada wa teknolojia kwa wachimbaji wadogo ili kuondokana na uchimbaji wa zana duni.“Mheshimiwa waziri mkuu mfano unaona mtambo huu umetolewa na serikali na tunaupeleka mgodi wa GGML kwa ajili ya kuchoronga ,kwani shirika letu linatoa huduma hiyo kwenye mgodi huo,” alisema Magala.Kwa upande wake Majaliwa baada ya kujionea teknolojia hiyo ikiwemo matumizi ya mtambo wa kutumia injini ya pikipiki amelipongeza shirika hilo la STAMICO ambalo limeonyesha nia ya kuwasidia wachimbaji wadogo kuondokana na matumizi ya zana duni na zebaki.Awali Mkuu wa mkoa wa Geita akitoa salamu za mkoa huo amesema uzalishaji wa madini ya dhahabu katika mkoa huo yameongezeka hadi tani 22.5 za madini kutoka kwa wachimbaji wadogo.


 

Comments