Mgombea ubunge Jimbo la Bukombe mkoani Geita Dkt. Doto Biteko amewaomba wananchi kuchagua mgombea Urais Samia Suluhu Hassan, madiwani na Mbunge wa CCM ili kupata maendeleo. Wito huo ameutoa kwenye mkutano wa kampeni Septemba 9,2025 akiwa kata ya Busonzo akitokea kata ya Namonge.
Dkt. Biteko akiwa Busonzo amesema Tanzania hii munayoiona vituo vikubwa vya kuzarisha umeme wa jua kwa kutumia jua kipo kimoja Kigoma kinazalisha umeme megawati tano kinarisha pale Kigoma mjini kituo kikubwa cha pili Serikali imeleta kata ya Busonzo kitazarisha megawati tano.
Amesema Idoselo inaingia kwenye ramani ya nchii hii kwa kuwa na mradi wa kuzarisha umeme mkubwa wa jua kwa mara ya kwanza lengo la Serikali ya CCM nikuhakikisha kila kaya inaumeme.
Dkt. Biteko amesema mradi wa maji kwenye kata hiyo umezidiwa hivyo baada ya uchaguzi atahakikisha mradi huo unapanuliwa na kutafuta chanzo kingine cha maji ili kusogeza huduma kwa wananchi.
"Busonzo Mambo mazuri yanakuja barabara najua zipo zingine tumezifungua zingine zimechoka kazi ya kwanza ilikuwa kufungua barabara kazi ya pili nikuimarisha barabara hata shule za msingi na sekondari zitaongezeka baada ya uchaguzi ukiwemo ujenzi wa Zahanati", Amesema Dkt. Biteko.
Uchaguzi Mkuu 2025 unahusisha na maendeleo yetu kura yako ni maendeleo nawaombeni Oktoba 29, 2025 nikuhakikisha tunatiki kwa Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kwa Diwani na kwa Mbunge wa CCM ili kupata maendeleo.
Mgombea udiwani kata ya Busonzo John Chubire wakati akiomba kura ameahidi kusimamia miradi ya maendeleo hivyo wa mpigie kura nyingi Dkt. Samia na Dkt. Biteko ili maendeleo yafike kwa wakati.
Wakazi wa kata ya Busonzo kwa nyakati tofauti Elizabet Paul amesema amefika kwenye mkutano huo kusikiliza sera na kudai kuwa sera amezielewa hasa Dkt. Biteko anavyo ongea kwa unyenyekevu akiomba kura licha ya kuleta maendeleo kwa miaka mitano iliyopita hakika anatosha.

Comments
Post a Comment