DKT. BITEKO AMUOMBEA KURA ZA KISHINDO MUGOMBEA URAIS DKT SAMIA


Na Ernest Magashi

Mgombea ubunge jimbo la Bukombe mkoani Geita, Dkt. Doto Biteko  amewataka wananchi wa kata ya Bukombe kupiga kura nyingi kwa Mgombea urais Dkt. Samia.Dkt. Biteko ameyasema hayo Septemba 12, 2025 kwenye mkutano wa kampeni kata ya Bukombe akiomba kura za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan  kwa wananchi amesema miradi ya maendeleo iliyotekelezwa ni mikubwa na baada ya uchaguzi Oktoba 29,2025 maendeleo yanakuja makubwa zaidi.

"miradi mingi inakuja hatua ya kwanza tulipeleka vipaumbele vya wananchi kwa kujenga shule za msingi na Sekondari, Zahanati pia kupeleka umeme vijijini hatua inayofuata nikufikisha kila kitongoji  umeme na kuhakikisha Zahanati zinajengwa nakuongeza madarasa na kuanzakufanya ukarabati wa madarasa", amesema Dkt Biteko.Akiomba kura za Rais na diwani, Dkt. Biteko amesema hatua ya kwanza tumepeleka shule ambapo hawakua na shule tukichaguliwa Oktoba 29,2025 tunaanza kukarabati shule zetu ili ziwe na muonekano mzuri.Akiomba kura mgombea udiwani wa kata ya Bukombe Rozalia Masokola alianza kwa kumpongeza Dkt. Biteko na Dkt. Samia kwa kazi kubwa ya kuleta maendeleo kata ya Bukombe.Masokola amesema kwa miaka mitano kuanzia 2020 hadi 2025 akiwa diwani amesimamia miradi mbalimbali ya Elimu, Afya na miradi migine ikohatua ya ukamirishaji ukiwemo mradi wa maji kwa miaka mitano mingine atahakikisha miradi mipya anaisimamia kwa ukamilifu. 

Comments