DKT. BITEKO AMESEMA MAENDELEO YAJAYO NIMAKUBWA ZAIDI

 

Na Ernest Magashi

Mgombea ubunge jimbo la Bukombe mkoani Geita ,Dkt. Doto Biteko  amewataka wananchi wa kata ya Butinzya kupiga kura nyingi kwa Mgombea Udiwani, Ubunge na Rais wa CCM kwa maendeleo. Dkt. Biteko ameyasema hayo Septemba 11,2025 kwenye mkutano wa kampeni kata ya Butinzya akiomba kura za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan  kwa wananchi amesema miradi ya maendeleo iliyo tekelezwa ni mikubwa na bada ya uchaguzi Oktoba 29,2025 maendeleo yanakuja makubwa zaidi.

"miaka ya nyuma hapakuwa na barabara, umeme ,shule ya sekondari na zahanati leo hatuzungumzi hayo tunazungumzia kuongeza miradi ya maendeleo na kuipandisha hazi zahahati kuwa kituo cha afya", amesema Dkt. Biteko. Amewaomba wananchi kupiga kura za kishindo  kwa Rais, Mbunge na Diwani na kwamba hatarajii kuona miradi inasuasua badalayake isimamiwe na ikamilike kwa wakati ili wananchi wapate huduma za Elimu, Afya na Maji maeneo ya karibu zaidi. "Butinzya haikuwa hivi haikuwa na barabara, leo kunamabarabara ya mefunguliwa na Serikali kwa usimamizi aliyekuwa diwani kabla ya Mgombea wa sasa nimpongezi amefanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo na sasa yanaenda kuja maendeleo makubwa bada ya kutiki Oktoba, 29, 2025 na mukimaliza kupiga kura nendeni nyumbani mengime tuachieni Sisi", amesema Dkt. Biteko. Akiomba kura mgombea udiwani wa kata ya Butinzya Kwizi Chenya alianza kwa kumpongeza Dkt. Biteko kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa miaka mitano ya kuwaletea wananchi maendeleo.Kwizi ameahidi kusimamia fedha za miradi ya maendeleo ili ikamilike kwa wakati kwa kushirikiana na Mbunge anaepambana kuibadirisha Bukombe. Wakazi wa kata ya Butinzya kwa nyakati tofauti wakiwa kwenye mkutano wakifatilia sera za wagombea Udiwani na Ubunge Rehema Juma, Paul Luhemeja.

Rehema amesema sera za wagombea amezielewa na Dkt. Biteko hanaga ahadi za uongo aliahidi umeme leo unawaka.

Paul amesema amefurahi sana kusikia wagombea wanaahidi kukamilisha Zahanati pia kukarabati miundombinu za shule ya msingi Butinzya itapendeza wing Oktoba 29,2025 tutatiki.


 
 

Comments