Mgombea Ubunge Jimbo la Bukonbe Dkt. Doto Biteko ameahidi baada ya uchaguzi kwa kushirikiana na diwani na wananchi kujenga shule ya sekondari yenye ambayi itapokea wanafunzi hadi wa kidato cha tano na sita kata ya Bulenga.
Dkt. Biteko ametoa aahadi hiyo kwenye mkutano wa kampeni kata ya Bulenga wakati akionba kura za mungombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Pia kupitia mkutano huo Dkt. Biteko amewashukuru wananchi wa kata ya hiyo kwa miaka mitano ambayo ameimaliza akiwa mbunge katika ushirikiano na wananchi pamoja na viongozi wote wa kata hiyo kwa mafanikio ambayo wameyapata.
Aliwaomba viongozi wa chama kusaka kura kwenye kata ya Bulenga, ambapo katika kata hiyo miaka ya nyuma hapakuwa na umeme, maji na katika sekta ya afya haikuwa nzuri na miundombunu za barabara hazikuwa zinalidhisha kwa wakati.
"Lazima Bulenga tuongeze shule katika kata hii kwasababu katika kata zingini shule za kidato cha sita zipo kwahiyo na hapa lazima iwepo mkimchangua Rais Dkt. Samia Suluhu Hasasan maendeleo hayo yatakuja maana wananchi hawataki maneno wanataka maendeleo, kama hutapiga kura, kura yako ndio uwekezaji wako na kura yako ni maendeleo yako,"alisema Dkt Biteko.
Aliongeza kuwa wilaya yetu ilikuwa nyuma lakini kwa sasa imebadilika kwa mambo ya kimaendeleo na sekta zote kwasasa zipo vizuri, pia kwasasa lami inawekwa kutoka Ushirombo hadi Katoro kwahiyo hakuna kitu ambacho Rais Dkt. Samia atamuomba na akatae endapo tutamchangua kwa kura nyigi ndio maendeleo ya jimbo la Bukombe watu wajitokeze kwenda kupiga kura Oktoba 29,2025.
Kwaupande wake mgombea udiwani Erick Kagoma ,amewashukuru wananchi wa kata ya Bulenga kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo, amesema katika kata yake hiyo ina mtandao wa umeme katika vijiji vyote.
Na jitihada za ujenzi wa barabara zinaendelea na katika sekta ya afya maendeleo yanaoneka hayo yote nijitihada kwa viongozi mahili Dkt. Biteko na Rais Dkt Samia.

Comments
Post a Comment