Mgombea ubunge wa jimbo la Bukombe kupitia chama cha mapindunzi (CCM) Dkt ,Doto Biteko ameahidi utekelezaji katika miradi ya maendeleo kata ya Iyogelo endapo wananchi watawapigia kura nyingi katika kata hiyo.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Iyogelo katika kampeni za kusaka kura za Rais Samia Suluhu Hassan ,ubunge pamoja na udiwani akinadi Ilani ya chama hicho katika miaka mitano iliyopita ,na katika miaka mitano ijayo ambapo itaielekeza kutekeleza miradi ya maendeleo.
Dkt, Biteko ameeleza jinsi utekelezaji huo utakavyofanyika katika miaka mitano ijayo endapo chama hicho kitapata ridhaa ya kuongoza tena,ameahidi kujenga Zahanati katika kitongoji cha Nyamankungwa,vitu vyote amesema atatoa endapo watapiga kura.
"Rais Samia ametufundisha ustaarabu mpya wa nchi hii kwamba tunaweza kuwavumilia watu wa aina yeyote ,acha mtu aseme chochote ,maendeleo yatatumiwa na wote yakiwepo maji watatumia,barabara hii haiulizi kabila wala chama wala dini, wale wanaotukana Mama amesema tusiwajibu ,"alisema Dkt Biteko.
Sambamba na hayo amesisitiza kuwa hakuna mchawi, mchawi ni elimu watoto waende shule ili wapate elimu ambayo baadaye itakuwa msaada wa baadae,kwahiyo watu wajitokeze kwenda kupiga kura maana jambo la kupiga kura ni jambo la muhimu kura yako ndio maendeleo yako.
Hata hivyo mgombea udiwani kata ya Iyogelo Juma Lushiku aliwashukuru wakazi wa Iyogelo kwa kujitokeza kwenye mkutano wa kampeni za kusaka kura za Rais ,ubunge pamoja na udiwani kwajinsi ambavyo wamejitokeza.
Vilevile alieleza vipaumbele ambavyo vinahitajika katika kata hiyo ya Iyogelo ameomba uboreshaji wa zahanati ambayo ilikuwa chini ya kiwango hapo Nyamankugwa, changamoto ya umeme katika vitongoji ambavyo bado havina umeme na miundombinu ya barabara.
Aidha alisema CCM ikipewa ridhaa ya kuongoza kwa miaka mitano ijayo itatekeleza miradi yote ambayo inatakiwa kutekelenzwa katika kata hiyo .

Comments
Post a Comment