DKT BITEKO- AHIMIZA WAPIGA KURA KUCHAGUA CCM KILA KITONGOJI UMEME UTAFIKA

 Na Irene Makopudo

Mgombea ubunge jimbo la Bukombe mkoani Geita Dkt. Doto Biteko  amewataka wananchi wa kata ya Katome kujitokeza kwa wingi  Oktoba 29, 2025 kumpigia kura Rais Dkt Samia Suluhu Hassan  kwa kuwa  anawapenda wananchi wa Bukombe. Dkt. Biteko ameyasema kwenye mkutano wa kampeni kata ya Katome ameeleza mafanikio ambayo yamefanikiwa kufanyika kwenye kata hiyo, amesema  miaka mitano iliyopita hapakuwa na barabara, umeme, hata shule ya sekondari. Ameongeza kuwa wananchi wakipiga kura nyingi zanisehemu ya maendeleo ya kupata fedha za miradi mbalimbali hasa kwenye barabara, Elimu na maji kwa kuganya utafiti wa maji.

Dkt Biteko amewashukuru wakazi wa kata hiyo kwa kujitokeza kwenye mkutano huo lakini amewahakikishia wakazi wa Katome  kwamba maendeleo lazima yaendelee kufanyika katika kata hiyo na kuwataka wakazi hao kujitokeza  kupiga kura Oktoba 29,2025.

Amesema wananchi bada ya uchaguzi licha ya umeme kufika kila kijiji atahakikisha kila kitongoji kinafikishiwa na umeme.

 Aidha mgombea udiwani wa kata ya Katome Joseph Maganga ameeleza maendeleo ambayo yamefanyika kata hiyo ni kwa nguvu za Mbunge Dkt Biteko na Rais Dkt Samia ambao inatakiwa tuwape kura nyingi siku ya kupiga kura.Maganga akiendelea kura za Mbunge Dkt. Biteko na Rais Dkt.Samia Alison shukrani kwa maendeleo ambayo wamepata katika kata ya Katome ,kwasasa maji yapo na umeme upo, aliwaomba wananchi wa Katome kwenda kupiga kura kwa wingi ili wapate maendeleo.

Mkazi wa Katome Pius Shija amesema nikweli Serikali imefanya Mambo makubwa zamani walikuwa wanatembea umbali mrefu wanafunzi kwenda sekondari, na kufata huduma za Afya, na maji.

Shija amesema kwa sasa changamoto hizo hazipo na vizuri zaidi wagimea Sera zao zinaeleza kunamaendeleo makubwa yanakuja ninaimani nao mimi nitapiga kura. 


 
 

Comments