Na Irene Makopudo
Mgombea ubunge jimbo la Bukombe ,Dkt. Dotto Biteko amewataka wananchi wa kata ya Ng'anzo Wilaya ya Bukombe Mkoani wa Geita kujitokeza kwa wingi Oktoba 29, 2025 kumpigia kura Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwa anania thabiti ya kuleta maendeleo.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni zake kata ya Ng'anzo katika ameeleza mafanikio ambayo yamefanikiwa kufanyika katika kata hiyo, amesema miaka ya nyuma hapakuwa na barabara ,umeme ,shule ya sekondari na zahanati.
Amesema wananchi wakipoga kura za kishindo Zahanati ya Ng'anzo ita pandishwa hadhi kutoka kwenye zahanati kuwa kituo cha afya.
Dkt Biteko amewashukuru wakazi wa kata hiyo kwa kujitokeza kwenye mkutano huo lakini amewahakikishia wakazi wa Ng'anzo kwamba maendeleo lazima yaendelee kufanyika katika kata hiyo na kuwataka wakazi hao kujitokeza kupiga kura.
"Ng'anzo haikuwa hivi haikuwa na barabara ,hapakuwa na sekondari watoto wengi walishindwa kuendelea na masomo kwa sababu ya umbali walishindwa kuendelea na shule wengi walibebeshwa mimba, hospitali ilikuwa shida wakati wamama wanakwenda kujifungua walikuwa wanajifungulia njiani wakiwa wanaenda hospitali nje ya kata", aisema Dkt Biteko
Ameongeza kuwa endapo mtampa diwani, Mungu Rais wa CCM ridha ya kuongoza tena maendeleo ni lazima ,miaka mitano itakuwa ya maendeleo ,mkoa mzima wa Geita Wilaya inayo ongoza ni Bukombe katika sekta ya elimu imeongoza kuanzia darasa la 4, darasa la 7 na sekondari hadi kidato cha 6 .
Awali mgombea udiwani wa kata ya Ng'anzo Mashaka Shing'wenda ameeleza maendeleo ambayo yamefanyika kata hiyo ,katika sekta mbali mbali zikiwemo miundombinu ya barabara kutoka Ng'anzo hadi Bulenga kilomita 6 na Barabara ya Mtakuja hadi Isemabuna kilomita 4, Mbagwa hadi Butinzya, Mtinga hadi Segwe na Bwenda.
Shing'wenda alimshukuru Dkt Biteko kwa maendeleo ambayo wamepata katika kata ya Ng'anzo ,kwasasa maji yapo na umeme upo, aliwaomba wakazi wa Ng'anzo kupiga kura kwa wingi.

Comments
Post a Comment