DE-D BUKOMBE AWAPONGEZA KINAMAMA WATATU WALIYOJIFUNGUA MAPACHA

Na, Henry Evarist 

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya Bukombe, Adelina Mfikwa amewapongeza kimama waliojifungua mapacha watoto watatu na amewaomba mama watatu hao kuendelea kuwatunza na kuzingatia ratiba za kliniki.Adelina Mfikwa ametoa wito huo leo Septemba 8, 2025 alipofika kituoni cha afya Uyovu kilicho pandishwa hadhi na kuwa hospitali akiongozana na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Dkt. Deograsia Mkapa na Mratibu wa afya ya uzazi (DRCHco), Masanja Nkola kwa lengo la kuwapongeza na kuwapatia zawadi mbalimbali zikiwemo nguo na mabegi.

“Kilichonivuta kuja hapa ni kitendo cha kuzaliwa mapacha watatu watatu (seti 3) katika kipindi cha wiki moja kwahiyo nikatamani kuja kuwaona hao akina mama kwani kuna wakati mwingine, mama anaona kama mzigo utakuwa mkubwa, ” alisema DED Adelina.Ameongeza kuwa wazazi hao wanahitaji faraja kutoka kwa watu mbalimbali pamoja na jamii inayowazunguka ili kuelendelea kukua vizuri mapacha hao.

Aidha, amefafanua kuwa pamoja na kutoa zawadi kwa mama waliojifungua mapacha watatu, wametoa zawadi pia kwa wazazi wengine wenye mapacha wawili na wenye mtoto mmoja waliojifungua ndani ya kipindi hicho.DED Adelina pia ametoa wito kwa jamii kuendeleza matendo ya huruma kwa watoto kwa kuwapatia misaada mbalimbali.

Akizungumza hospitalini hapo, Mganga Mkuu wa halmashauri, Dkt. Deograsia Mkapa amewataka wazazi wote kuzingatia malezi kama ambavyo wamefundishwa katika maudhurio ya kliniki.Dkt. Mkapa ameihasa jamii kuepuka imani potofu kwa kuamini kuwa wanapozaliwa watoto wawili au watatu (mapacha) kama ni laana au mkosi kwenye familia au kwenye jamii.

“Siyo mkosi, kisayansi inawezekana, na tafiti zinaeleza kwanini inatokea hivyo ikiwemo sababu za vinasaba, eneo la kijiografia, upandikizaji nakadhalika,” amesema Dkt. Mkapa. 

Pamoja hayo, amekiri ugumu ulipo katika kutunza mapacha watatu endapo mama ataachwa mwenyewe bila msaada kutoka kwenye familia na jamii inayomzunguka.

“Watoto waudhurie kliniki na kupata chanjo zote kama miongozo onavyosema” amesema Dkt. Mkapa.Mganga mfawidhi kituo cha afya Uyovu, Dkt. Timotheo Masepa amesema kuwa afya za watoto hao zinaendelea vizuri na wazazi walijifungua kawaida bilachangamoto yeyote katika kituo hicho chenye rekodi ya kuzalisha watoto kati ya 350 hadi 450 kwa mwezi.

Akishukuru kwa niaba ya wazazi wenzake waliopatiwa msaada, Agnes Anthony ambaye mara ya kwanza alijifungulia kituoni hapo mapacha wawili na sasa mapacha watatu ameshukuru uongozi wa halmashauri pamoja na kituo cha afya Uyovu kwa huduma nzuri na kujali.

 

Comments