Na, Ernest Magashi
Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata wamewaomba wagombea wanaochukua fomu za kuomba ridha kwa wananchi kujaza fomu kwa usahihi na kurejesha kwa wakati ili kwenda na kareda ya uchaguzi. Wito huo umetolewa na wasimamizi wa saidizi wa uchaguzi ngazi ya kata mbalimbali wilayani Bukombe mkoani Geita walipokuwa wanapokea wagombea walioteuliwa na Chama Cha Mapinduzi CCM kata 17 ili wapepelushe bendera na kupigiwa kura na wananchi Oktoba 29, 2025.Msimamizi msaidizi kata ya Uyovu Ramadhan Ng'oi akimkabizi mgombea udiwani kata ya Uyovu Matayo Kagoma alitoa Elimu ya uchukuaji fomu kwa mgombea ili asikose anapo jaza fomu.
Mgombea udiwani wa kata ya Igulwa Richard Mabenga alisema baada ya kuchukua fomu kuwa amekuwa diwani tangu 2015 hivyo akichaguliwa na wananchi ameweka vipaumbere ambavyo ni kuboresha miundombinu ya barabara, huduma za afya, na maji kwa kutekeleza ilani ya CCM.
Naye mgombea udiwani kata ya Uyovu Matayo Kagoma alisema baada ya kupigiwa kura Oktoba 29,2025 atahakikisha anatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kwa kushirikiana na wanachama na wananchi kuleta mabadiriko ya kimaendeleo.
Aliwaomba watalamu kushirikiana kwa karibu ili kufikia malengo ya chama ikiwemo kupanua huduma za Afya na kuongeza ma barabara, huku mtandao wa maji kuwafikia wahitaji utaongezeka na vitongoji vyote vitawaka umeme. Kagoma akitaja vipaumbele vyake hivyo atakavyo fanya kwa miaka ameongeza kuwa kushirikiana na kipenzi cha wanabukombe Dkt. Doto Biteko na Rais Samia Suluhu Hassan kata ya Uyovu inatakiwa kuogezwa zahanati ili kupunguza msongamano wa wananchi kwenye kituo cha afya ambacho kilipandishwa hadhi kuwa hospitali ya Uyovu.
Pia alisema kunashule zinaupungufu wa madarasa kwa kutekeleza ilani madarasa yataongezwa na changamoto za wafanyabiashara wa mazao ya biashara atawatafutia frusa za masoko zikiwemo mboga mboga nyanya.
Mgombea wa udiwani kata ya Namonge Mlalu Bundara baada ya kuchukua fomu aliaza kwa kuipongeza Serikali kwa kuleta fedha nyingi za miradi ya maendeleo nakudai kuwa akichaguliwa ataedelea kusimamia miradi ili kusogeza huduma kwa wananchi. Bundara alisema kipaumbele chake ni kuboresha huduma za Afya, mabarabara na kusambaza maji na umeme licha ya kwamba huduma hizo zote zilishawafikia asilimia kubwa.
Naye mgombea udiwani kata ya Katente Tabu Kasuluzu Ng'hwani alisema anampongeza sana mgombea ubunge Dkt. Doto Biteko na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za miradi ya maendeleo kwa miaka mitano hivyo akichaguliwa na wananchi kwa miaka mitano atahakikisha fedha inayoletwa na Serikali anaisimamia kikamirifu ili wananchi waendele kufurahia Serikali ya CCM.
Pia mgombea udiwani kata ya Butinzya Kwizi Chenya Mathias aliaza kwa kuwashukru wanachama wa CCM kwa kumpa kura za kutosha ili apeperushe bendera ya chama na kutekeleza ilani ya CCM kuwaletea maendeleo wananchi wa Butinzya.
Akielezea vipaumbele vyake Kwizi alisema atasimamia fedha za miradi ya maendeleo na wananchi wawetayari kupokea miradi hiyo inayoletwa na Serikali bila kujali idikadi ya vyama vingine hivyo wananchi wote watanufaika kwa pamoja Butinzya ni ya Dkt. Doto Biteko na Rais Samia Suluhu Hassan.
Msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Katente Issa Msole akimkabizi fomu mgombea wa Udiwani kupitia chama cha mapinduzi CCM alisisitiza Mgombea kwenda kujaza fomu na kurejesha kwa wakati na kuabatanisha ratiba ya kampeni.
Comments
Post a Comment