RAIA WENGINE 20 WA KIGENI WAKAMATWA GEITA

Na, Ernest Magashi

Raia wengine 20 wa kigeni kutoka nchi jirani za Burundi na Uganda  mkoani Geita wamekamatwa baada ya kuingia nchini kinyume cha sheria.Idadi hiyo inafikisha jumla ya raia wakigeni 331 ambao wamekamatwa ndani ya kipindi cha miezi miwili mwaka 2025.Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Geita Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Donald Lyimo amesema  kukamatwa kwa raia hao ni sehemu ya operesheni ambayo inaendelea kufanywa na idara hiyo usiku na mchana.

Amesema raia hao walikuwa wameingia nchini kwa madai ya kutafita  ajira kwenye mashamba ya kilimo cha nanasi wilayani Geita, ndani ya mwezi huu wa Agost wamekamatwa raia 19 kutoka nchini Burundi na raia mmoja kutoka Uganda. 

Raia hao kwa nyakati tofauti tofauti wameeleza kuwa wanavuka mipaka kutokana na changamoto mbalimbali za nchini mwao ikiwemo za kiuchumi. Lymo akitoa with kwa jamii kuendelea kutoa taarifa za raia wa kigene idara ya uhamiaji itaendelea na operesheni za kuwakamata wahamiaji na kuwarudisha nchini kwao. 


Comments