DKT. MKAPA ACHAGULIWA TENA KUWA MRATIBU WA MEWATA

Na, Henry Evarist 

Mganga Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Bukombe, Dkt. Deograsia Mkapa, (MD,MSc Field Epidemiologist) amechaguliwa kwa kura zote za ndio kuendelea kutumikia Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (Medical Women Association of Tanzania- MEWATA) kwa nafasi ya mratibu wa kanda zote, (National Zonal Chapter Co ordinator). Uchaguzi huo ulifanyika Jijini Arusha Agosti 23, 2025 wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama hicho katika ukumbi wa Gran Melia.Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe kama mwanachama na aliyewahi kuwa kiongozi wa chama hicho.Dkt. Mkapa alipata kura zote za ndiyo kutoka kwa wanachama (Wajumbe) wa mkutano Mkuu wa chama cha madaktari wanawake Tanzania (MEWATA) wapatao 90 kutoka kanda zote.

Akizungumza na mwandishi wetu mara baada ya ushindi huo mbali na kukiri kuwa ni heshima kwa wanabukombe wote, Dkt. Mkapa alisema “Nawashukuru sana wanachama na ninaahidi kuendelea kufanya kazi kwa weredi hasa eneo la afya ya wanawake na watoto," alisema.Katika uchaguzi huo, Dkt. Mkapa  alikuwa anagombe kipindi chake cha pili ambapo ameyataja mafanikio katika kipindi chake kama kiongozi wa MEWATA amefanikiwa kupata wanachama kwa kanda zote na kwa mara ya kwanza chama kikipata wanachama 18 kutoka Zanzibar.

Dkt. Mkapa alisema MEWATA ilianzishwa mwaka 1987 na kusajiliwa kama shirika lisilo la kiserikali Oktoba 1989 na Chama hicho kinawaunganisha madaktari wanawake wa tiba na meno kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Alisema dira ya chama ni kuhakikisha Madaktari wanawake waTanzania wanang'ara katika maadili ya kitabibu na meno kwa kufikia taaluma bora ya afya.

Pia alitaja adhima ni kuendeleza maendeleo ya kitaaluma kwa wanawake walioko katika taaluma za tiba na meno, ili kuwawezesha kutoa huduma bora za afya kwa wanawake wa Tanzania.


Comments