DKT. DOTO BITEKO ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA BUKOMBE

Na, Ernest Magashi

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Zedekiah Solomon Osan amemkabidhi fomu ya uteuzi wa kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Bukombe mgombea umbunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Doto Mashaka Biteko leo Agosti 26, 2025 katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wilaya ya Bukombe. Kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka 2025 Maelefu ya wana CCM na wapenzi wa chama hicho wamemsindikiza mgombea kwa ajili ya kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea umbunge zaidi ya wanachama 1000 wamejitokeza kumdhamini Dkt. Biteko ikilinganishwa na mahitaji ya wadhamini 31 waliohitajika kisheria.Akizungumza na wana CCM katika viwanja Ofisi ya CCM Wilaya ya Bukombe, Dkt. Biteko amewataka wananchi na wanachama kudumisha mshikamano na upendo miongoni mwao ili kuwachagua viobgozi bora.“Utakapofika wakati tuwachague viongozi tunaowapenda, pia nawaomba mmchague Dkt.  Samia Suluhu Hassan kuwa Rais, Mnichague mimi kuwa mbunge na niwaaombe mniletee madiwani wa CCM ili tuendeleze kazi tulizokwisha zianza,” amesema Dkt. Biteko.Katibu wa CCM, Wilaya Bukombe Leonard Mwakalukwa amesema wana CCM zaidi ya 3500 wamejitokeza kumsindikiza mgombea ubunge katika Ofisi za tume huru ya Uchaguzi kwa ajili ya kuchukua fomu.

Mwakalukwa alieashukru wanachama na wananchi kwa kunitokeza kwa wingi kwa kuonyesha mahaba makubwa kwa mgombea ubunge na wadhamini 31 kutoka Kata zote 17 za Bukombe wamewawakilisha wenzao 969.


Comments