Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambae mgombea peeke ndani ya chama cha mapinduzi CCM Dkt. Doto Biteko amewafikia wana CCM na kuomba kura kila kata.Dkt. Biteko ambae ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati aliaminiwa na wana chama na wananchi kuwa muwakirishi wao tangu 2015 kwa kupata kura nyingi.Akiomba tena ridhaa ndani ya chama Dkt. Biteko ameeleza furaha na shukrani aliyonayo kwa Wananchi wa Bukombe kufuatia ushirikiano waliompa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Dkt. Biteko amewaomba wananchama Agost 2, 2025 wafike kwa wingi kwenye maeneo ya kupigia kura wakachaguwe madiwani ambao wataona wanafaa na yeye wampe kura nyingi za ndiuo kutokana na kumwamini haliambayo imepelekea kuwa mgobea pekee.
"Wanachama wezangu nawaombeni sana na juwa nyinyi niwatu wema mtachagua munaeona anafaa asiwepo mgombea udiwani kwenye jimbo hili anasema nimetumwa na Doto Biteko hapana wapimeni kwa Sera zao na atakae pita tukutane bada ya kura za chama kuleta maendeleo kwa wananchi poa namuombea kura nyingi Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Hayo ameyazungumza kwa nyakati tofauti tofauti akiomba kura kuanzia kata ya Bukombe, Lyambamgongo, Bugelenga, Iyogelo, Ushirombo, Namonge, Busonzo, Uyovu, Runzewe Magharibi, Runzewe Mashariki, Bugelenga, Ng'anzo, Butinzya, Katome, Bulangwa,Katentena Igulwa.
Dkt. Biteko alisema wakati anagombea ni tofauti na sasa 2015 mtandao wa barabara umeongezeka kutoka kilomita 259 hadi kilomita1,445 na Sekta ya Elimu tunaongoza kwa kuwa na shule nyingi za Msingi na Sekondari tofauti na ilivyokuwa Mwaka 2015.Alisema shule za msingi na sekondari zimeongezeka zahanati na vituo vya afya vimeongezeka huku kituo cha afya kikipandishwa hadhi kuwa hospitali ya Wilaya shule za sekondari kidato cha tano na Sita mwaka 2025 tunazo shule TANO naimani Serikali itaendelea kuleta miradi mbalimbali na fedha nyingi za kuboresha huduma za afya katika wilaya yetu ya Bukombe.Dkt.
Biteko amesema kuwa dhamira yake kwa Wanabukombe ni Maendeleo na wakati wote anafikiria kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kwa Wananchi wote kwa kushirikiana na Serikali kufungua barabara."Moyoni mwangu ninalo deni kubwa sana la kufanya kazi zaidi kutokana na heshima ambayo wanachama na wananchi wameendelea kunipa wakati wote naombeni muendele kuniamni munitume nikafanye kazi ya kuleta maendeleo," alisema Dkt. Biteko.
Pia diwani ambae amekuwa mgombea pekee kata ya Katente Kasuruzu Ng'hwani alisema Dkt. Biteko nihakiyake kuwa mgombea pekee ndani ya chama amewafanyia Mambo mengi wananchi wanna maendeleo na miradi ambayo imekuwa ikiletewa fedha na serikali wananchi wanaona amekuwa kiongozi wa kila mara ana ludi jimboni kuhamasisha maendeleo kwa wananchi analudi tena Bungeni.Prisca Charles Amesema na vijana kata ya Igulwa waliongana na wanachama wakisema tu naimani na Dkt.Doto Biteko na tunatambanae hakika amefanya maendeleo makubwa ikiwemo kuwaunganisha wananchi na kuhamasisha wananchi washirikiane na Serikali katika miradi ya maendeleo.
Comments
Post a Comment