Mgombea pekee ubunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Mashaka Biteko ameshiriki kupiga kura za maoni kwa nafasi ya Ubunge na Udiwani katika kata ya Bulangwa.
Dkt. Biteko akiwa ukumbini pamoja na wajumbe wengine wa mkutano mkuu wa kata ya Bulangwa wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Mjumbe wa kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya Wilaya, Ndugu Mlagiri kuelekea kupiga kura za maoni katika nafasi ya Udiwani na Ubunge Jimbo la Bukonbe, Mkoani Geita.
DKT. Biteko ametumia hakiyake ya kupigia kura za maoni kmpata Diwani huku mbune akiwa mgombea pekee akipiga kura ya ndiyo.
Msimamizi wa Uchaguzi kwenye kata hiyo Paskasi Mlagiri Mjumbe wa kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Bukombe, Agosti 4, 2025, Mkoani Geita.

Comments
Post a Comment