Askari wanne wa Jeshi la uhifadhi wilayani Bukombe mkoani Geita wanashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za mauaji ya mkazi wa kijiji cha Msonga wilayani Bukombe.
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Geita Adam Maro amemtaja mtu huyo aliyefariki kuwa ni Eziboni Fikiri, mkulima mwenye umri wa miaka 20.Maro amesema tukio hilo limetokea Agosti 13,2025 majira ya saa 12 asubuhi wakati askari hao wakikamata wananchi ambao walikuwa wamevamia pori la hifadhi la Kigosi.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Bukombe kwaajili ya uchunguzi wa kitaalmu. Aidha watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa na jeshi la polisi na uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
Hata hivyo jeshi la polisi mkoa wa Geita limewasihi wananchi kuwa watulivu wakati uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea kufanyika ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa wahusika kwa mjibu wa sheria.
Mkazi wa Msonga wilayani Bukombe Martha John amelipongeza jeshi la polisi kwa kuwashikiria Askari hao wa uhifadhi na halihiyo inaumiza sana wananchi.
Comments
Post a Comment