Na, Ernest Magashi
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko ameendelea kuboresha huduma kila idara Wilaya ya Bukombe ambapo aliwaomba Kampuni ya Airtel kuleta vifaa vya kusambazia mtandao wa Internet wa 5G katika Shule za Sekondari ili kurahisisha utoaji wa elimu kwa njia ya mtandao.
Awamu ya kwanza imehusisha shule 10 zikiwepo shule zote za kidato cha tano na sita.
Hayo ameyasema Afisa Takwimu na vifaa shule za sekondati Wilaya ya Bukombe Leonard Nkingwa kwa niaba ya Afisa Elimu Wilaya ya Bukombe.
Nkingwa ameishukuru kampuni ya Airtel Tanzania kwa kuisaidia Wilaya ya Bukombe katika kuimarisha upatikanaji wa Elimu kwa njia ya mtandao ikiwa ni pamoja na kupata materials za kufundishia.
Meneja wa Airtel Tanzania Mkoa wa Geita bwana Joseph Mushi akieleza dhamira ya kutoa mafunzo ya kutumia mtandao katika kujifunza shuleni kwa Wakuu wa Shule pamoja na walimu wa TEHAMA ameeleza nia na dhamira ya Airtel kuendelea kutoa kwenye jamii na hasa eneo hili ili kuzalisha kizazi kinachoendana na Sayansi na Teknolojia.
Comments
Post a Comment