Jumla ya raia wa kigeni 126 kutoka nchi jirani ya Burundi wamekamatwa na idara ya uhamiaji mkoani Geita na kuwarudisha makwao baada ya kuingia nchini Tanzania kinyume na taratibu. Akizungumzia Oparesheni hiyo katika Ofisi za uhamiaji zilizopo Magogo Mkoani Geita Kamishina msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Mkoa wa Geita James Mwanjotile amesema wahamiaji hao wamekamatwa maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Geita.
Kamanda Meanjotile alisema hadi Juni 30,2025 Idara hiyo imefanikiwa kuwakamata na kuwarejesha makwao raia wa kigeni 593 idadi kubwa ni kutoka Taifa la Burundi na wengine kutoka mataifa mengine ya Afrika Mashariki.Kamanda Mwanjotile amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na Idara hiyo pamoja na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kukabiliana na uingiaji holela wa raia wa kigeni.
Kwa upande wao baadhi ya raia hao wa Burundi Ndaijimana Helodi na Bizimana Gerlad waliokamatwa.
Helodi alisema walingia nchini Tanzania katika harakati za utaftutaji wa maisha huku Gerlad akielezea kuwa alikuja na wezake kutafuta maisha sasa wamekamatwa hawana chakufanya.
Comments
Post a Comment