Jeshi la polisi Mkoa wa Geita limewataka madereva wa vyombo vya moto vya kusafiria watu kuendelea kuwa makini wanapokuwa barabarani sambamba na kupata muda wa kupumzika baada ya kuendesha vyombo hivyo kwa safari na muda mrefu.
Wito huo umetolewa na Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Geita Safia Jongo wakati akidhibitisha ajari ya watumishi wawili wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA Mkoa wa Mwanza kufariki dunia baada ya kupata ajari eneo la Bwawani barabara ya Katoro wilayani Geita mkoani Geita wakiwa wanatokea Mutukula mkoani Kagera.
Jongo amesema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia julai 20 majira ya saa 10:00 usiku baada ya dereva wa gari mali ya TRA lenye namba za usajili STM 3696 Bw. Julius Dismas (31) kuwa na uchovu na kushindwa kulimudu gari hilo.
Kamanda Jongo amewataja waliofariki dunia katika ajari hiyo ni Afisa forodha Emmanuel Leonard (33) na
Afisa forodha Mwita John (28) wote wakazi wa Buswelu wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
Comments
Post a Comment