DKT. BITEKO AWAPONGEZA WATENDAJI WIZARA YA NISHATI NA TAASISI ZAKE WAIMARIKA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 95


Na, Ernest Magashi

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewapongeza Watendaji wa  Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa kuendelea kuimarisha utendaji kazi na hivyo kuifanya Sekta ya Nishati kuwa na matokeo chanya katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Dkt. Biteko ametoa pongezi hizo kufuatia tathimini ya utendaji kazi iliyofanywa na Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathimini katika Wizara ya Nishati ambayo imeonesha kuwa katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2024/2025 utendaji kazi  wa Wizara na Taasisi umeimarika kwa zaidi ya asilimia 95.
Katika kikao cha Nne cha tathmini ya utendaji kazi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake kilichofanyika jijini Dodoma, Dkt. Biteko amesema kuwa, tathmini hiyo inasaidia  kujiimarisha hasa ikizingatiwa kuwa Sekta ya Nishati ina muhimu mkubwa kiuchumi na kijamii.

“Sekta hii ni muhimu sana nchini kwa kuwa ni Sekta ya huduma na sekta ya uchumi hivyo ikilegalega italeta malalamiko, ningependa kuona sekta hii inaendelea kuwa na matokeo mazuri kwa wananchi.” Amesema Dkt. Biteko

Katika kikao hicho, Dkt. Biteko ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuendelea na kasi ya ukarabati wa miundombinu ya umeme pamoja na kuendelea kutafuta vyanzo vipya vya umeme.

Aidha, amemupongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kwa kazi aliyofanya ya kupeleka umeme vijijini na kuwezesha vijiji vyote kupata umeme pia kwa kuendelea na kasi ya kupeleka umeme vitongojini.

Kuhusu Nishati Safi ya Kupikia, Dkt. Biteko amezitaka Taasisi zilizo chini ya Wizara hususan, REA, TPDC na TANESCO kuunganisha nguvu katika kutekeleza Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia ili ikue na kufanikiwa na hivyo kutimiza lengo la Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha kuwa wananchi wanahama kutoka matumizi
                    

Comments