WANNE WAJERUHIWA BAADA YA BULLDOZER KUJIENDESHA NA KUGONGA NYUMBA GEITA, DEREVA AINGIA MITINI

 

Watu wanne wakazi wa kitongoji cha Isangilo kata ya Lwamgasa wilayani Geita mkoani Geita wamejeruhiwa pamoja na  nyumba tatu kubomoka na uharibifu wa ngunzo ya umeme  baada ya mtambo unaotumika katika shughuli za uchimbaji wa madini wa mgodi wa BUCKREEF kusababisha ajali

Kwa mjibu wa taarifa ambayo imetolewa na jeshi la polisi mkoa wa Geita,mtambo huo(Bulldozer) wenye namba za usajili BGC –BD-002 ulisababaisha ajali hiyo baada ya dereva wake kuutekeleza alipohisiwa kuiba mafuta

Ajali hiyo imetokea Aprili 2 majira ya saa mbili usiku baada ya dereva alietmbulika kwa majina ya Ramadhan Samson kufuatiliwa na walinzi aliutelekeza mtambo huo na  kuanza kujiendesha wenyewe na kugonga nyumba tatu na kusababisha majeraha kwa watu hao

Jeshi la polisi mkoa wa Geita limesema waliojeruhiwa ni Pauline Charles (35) na mtoto Majaliwa Charles mwenye umri wa wiki mbili na wanapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Geita na wengine ni Philipo Ngh’abi (14) na Musa Michale (09) ambao waliruhisiwa baada ya kupata matibabu ya michubuko midogo

katika tukio hilo watuhumiwa wawili wamekamatwa na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ikiwemo kumtafuta dereva wa mtambo huo kwa hatu nyingine za kisheria

Comments