KANISA LA UFUNUO WAPELEKA MKONO WA POLE WAGONJWA NA WAUNGUZI WAPONGEZA BARIADI


Na, Ernest Magashi 

Wagonjwa na waunguzi hospitali ya Wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu wameupongeza uongozi na waumini wa wa kanisa la Ufunuo Bariadi makaomakuu ya jimbo la Simiyu kwa kutenga muda wa kuwatembelea wagonjwa na kuwapa mkono wa pole wa vitu mbalimbali sehemu ya mahitaji.
Miongoni mwa wagonjwa Joseph Jonathan baada ya kupokea mkono wa pole na mahitaji yake toka kwa Askofu wa kanisa la Ufunuo Jimbo la Simiyu Paschal Bendera.

Jinathan aliaza kutoa shukruni kwa kanisa la Ufunuo kuwa na viongizi wa kujari watu bila ubaguzi na kuongeza kuwa Askofu alichotoa  Mungu amsaidie aendele kusaidia watu hakika Mungu atamubariki kwenye kazi zake za kumtumikia Mungu niwachache wenye moyo wa kutembelea wagonjwa wengi wamekuwa wakitaka wafatwe ma kanisani.  
Naye Atirida Musima akiwa anasubiri kujifungua hospitalini hapo alimushukuru Askofu Paschal kwa kuja kuwatembelea na kuwapa pole na msaada wa vitu mbali mbali ambavyo wengine nimahitaji yakiwemo mabeseni na sabuni na yeye alikuwa nisehemu ya wahitaji.
Mwinjilisiti wa kanisa la Ufunuo Bariadi Pendo Kisinza alisema amebarikiwa sana na kitendo alicho kifanya Askofu Paschal amejifunza upendo binafisi amebarikiwa sana kufika hospitali kushiriki.

Katibu wa Jimbo la Simiyu Mariam Evarist akitoa shukrani kwa uingozi wa hospitali ya Wilaya kwa kuwa poke a vizuri. 

Mariamu alisema amejifunza vingi kutoka kwa Baba Askofu Paschal likiwemo hili tukio la kutoa mkono wa pole kwa Wagonjwa na wazazi binafisi nimejifunza kitu kikubwa sana kwa Askofu kwa tendo la huluma alillolifanya la kutembelea hospitali ya Wilaya kuona Wagonjwa. 

Grece Wiliamu mama mchungaji wa kanisa la EAGT kasoli alishukuru kanisa la Ufunuo kuarikwa kushiriki kwenye jambo kubwa la upendo lililofanywa na kanisa la Ufunuo. 

Mama Askofu jimbo la Simiyu Ester Doto alisema amefarijika na kupendezwa sana na Baba Askofu kutushirikisha kuja kusalimia wagonjwa ndugu najama waliolazwa. 
"Binafisi mimi nimependezwa na kitendo cha kuja kutembelea Wagonjwa na kuwatia Moyo na kuwapa hongera wasazi ", alisema mama askofu.

Mama Askofu Ester aliwaomba waumini kuendelea na umoja huo ili waendele kufanya kwa moyo mmoja kwa kufata misingi ya Baba Askofu. 

Muuguzi Mkuu wa hospitali ya Wilaya ya Bariadi  Rosemery Chiristopha akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu Mfawidhi wa hospitali ya Wilaya ya Bariadi alisema kanisa la Ufunuo Mungu awabariki kwa kufika kutembelea wagonjwa na kuwapa faraja ya vitu mbali mbali sehemu ya mahitaji.

"Tunawakaribisha sana tena sana wagonjwa wamefurahi na Sisi waunguzi tumefurahi kwa faraja ya Askofu Paschal hakika umefanya janbo kubwa sana tunawakaribisha tena ", alisema Muuguzi Mkuu.

Askofu wa kanisa la Ufunuo Jimbo la Simiyu Paschal Bedera alianza kwa kuwa pongeza waunguzu kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhudumia wagonjwa usiku na mchana. 

Askofu Paschal aliipongeza Serikali kwa kuendelea kuboresha miundombinu za hospitali Majengo yameongezeka  madawa na vifaa tiba vipo wagonjwa wanaifurahiya Serikali yao kwa kuwajali wananchi. 
"Mimi Askofu wa kanisa la Ufunuo Jimbo la Simiyu Paschal Bendera kwa kushirikiana na wachungaji na waumini wa kanisa la mahari pamoja nimekuja kutoa mkono wa pole kwa wagonjwa vile Mungu alivyo niongoza ninahakika kwa mkono huo kwa wagonjwa Mungu atatenda atawaponya", alisema Askofu  Paschal Bendera. 

Askofu Paschal aliongeza kuwa wametembelea wagonjwa mbalimbali kwa kugawa sabuni za unga, miche, na sabuni za watoto wachaga, mafuta ya kupaka watoto na wagonjwa watu wazima pia kila mgonjwa amepokea beseni  la kuongea na kufuria kuazia wodi ya mama na mtoto na wazazi wodi zote lengo ni kuwapa pole.
 

  

Comments