WATATU WAKAMATWA GEITA, WAKITOROSHA DHAHABU ‎GRAMU 3263

 

Na, Ernest Magashi

Geita. Watu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Geita baada ya kukamatwa na gramu 3263.72 za dhahabu yenye thamani ya shilingi milioni 749.5 ikisafirishwa kimagendo 

‎Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita ACP Adam Maro akitoa taarifa kwa wandishi wa habari amesema waliokamatwa ni Yohana Idama (34) mkazi wa Nyamhongolo wilayani Ilemela mkoani Mwanza, Moshi Manzili (26) mkazi wa Bariadi Simiyu na Hamidu Salum(25) mkazi wa Nyasubi wilayani Kahama mkoani Shinyanga

‎ACP Maro amesema watu hao walikamatwa machi 24,2025 majira ya saa tano usiku katika mtaa wa Kapera wilayani  Bukombe wakiwa na gari aina ya Toyota Premio lenye namba za usajili T. 739 EEH mali ya Emanuel Kidenya mkazi wa Kahama Shinyanga 

‎Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea kufanyika kwa kushirikina na mamlaka nyingine na uchunguzi ukikamilika, watakaobainika kujihusisha na uhalifu huo watafikishwa mahakamani
 

Comments