WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI GOLDLAND WATOA MAHITAJI KWA WAHITAJI HOSPITALI YA WILAYA YA BUKOMBE NA KUSHIRIKI ZOEZI LA USAFI WA MAZINGIRA
Na Henry Evarist
Wanafunzi wa sekondari ya Goldland wamefanya usafi katika maeneo mbalimbali ya hspitali ya wilaya Bukombe na kutoa msaada kwa wagonjwa waliolazwa ikiwemo matunda, sabuni, pamoja na fedha tasilimu.
Pia, baadhi ya wanafunzi hao walijitolea kuchangia damu jambo ambalo mganga mfawidhi wa hosiptali hiyo, Dkt. Yohana Fumbuka alisema ni muhimu katika kuokoa maisha ya binadamu.
Dkt. Funbuka amewataka wananchi pamoja na taasisi mbalimbali ndani na nje ya wilaya ya Bukombe kuiga mfano huo.
“Uhitaji wetu ni mkubwa. Kitendo cha wanafunzi hawa kujitolea kusaidia kufanya usafi ni jambo kubwa. Hata mtu akijtolea kuokota karatasi moja ni msaada mkubwa. Lakini hata kuwasalimia wagonjwa wanafarijika”
Aliongeza kuwa wanafunzi wamepata pia wasaha wa kujifunza jinsi kazi za hosipitali zinavyofanyika.
“Tumefurahi kwa shule kama shule kufikilia kutembelea hospitali ya wilaya na kutoa misaada mbalimbali” alisema Dkt. Fumbuka.
Aidha, alitaja utaratibu unatakiwq kufuatwa ili kutembelea hospitali hiyo kwa ajili ya matendo ya huruma kuwa ni kuandika barua ya kuutaarifu uongozi juu ya kusudio ili kuwawezesha kuqndaa vifaa muhimu kama glavuzi na barakoa au vizolea taka endapo ndilo lengo lao maana kila kundi lina malengo tofauti wengine wakitaka kutembelea tu wodi ya wazazi.
Pia alipongeza utamaduni uliopo kwa watu na makundi mbalimbali wakiwemo wanafunzi kujitolea kuchangia damu kutokana upungufu mkubwa uliopo ambapo kwa mwezi hospitali hiyo inahitaji Unit 160.
Kwa upande wake Afisa Muuguzi Msaidizi, Days Shem amepongeza hatua ya wanafunzi wa Goldland kufika hospitalini hapo akijihisi kuthaminiwa kupitia ushiriki wa jamii.
“Ni jambo zuri kuona jamii tunayoihudumia inatambua mchango wetu na kuja kushiriki katika shughuli tunazozifanya” alisema Days.
Aliongeza kuwa, pia ujio wa wanafunzi hao hospitalini hapo ni chachu na njia mojawapo ya kuwahamasisha kujiunga na fani ya utabibu baada ya kuona jinsi kazi hiyo inavyofanyika.
Mkuu wa shule ya sekondari Goldland, Mwl. Singu Kashinje alitaja lengo la kutembelea hospitali kuwa ni kujiungamanisha na jamii na pia kuwatia moyo wagonjwa ambao wengine maisha yao yamekuwa ni ya hospitalini kutokana na changamoto za kiafya na hivyo kuhitaji faraja.
“Sisi lengo letu kubwa ni kuja kuwatia moyo na kuwaasa kutokata tamaa na kutambua kuwa jamii wakiwemo wanafunzi bado wanawakumbuka na kuwaombea “ alisema Kashinje.
Alitaja faida mojawapo kwa wanafunzi kuwa ni kujifunza moyo wa uzalendo, kujitoa na kujali wahitaji.
“Tumeiga mfano kwa Mbunge wetu wa Bukombe, Dkt. Doto Biteko. Kwakweli anajitoa kusaidia jamii na kweli amejiungamanisha na jamii kiasi kwamba kila sehemu yupo. Kupitia kaulimbiu yake ya Kusema na Kutenda, tumehamasika kama shule kutenda tulichotenda leo” alisema Mwl. Mkuu Goldland, Kashinje.
Mwanafunzi Warda Mponzi wa kidato cha tatu aliupongeza uongozi wa shule pamoja na hospitali kwa nafasi waliyoipata kwa madai kuwa imemfanya kujihisi mmoja wa wanajamii kwa kushiriki usafi, kuzungumza na wagonjwa pamoja na watoa huduma za afya.
“Nimejifunza vitu mbalimbali ikiwemo namna ya kuishi na watu vizuri hasa baada ya kutembelea wodi mbalimbali ikiwemo sehemu ya kuhifadhia mahiti (mortuary) ambapo nimejifunza mwili unavyohidhiwa mtu akishakufa“ alisimulia Mwanafunzi mwingine wa kidato cha tatu, Fatna Kayombo.
Na Daudi Samson alisema kitendo cha kufika hospitalini hapo kimempa hamasa na moyo wa kusomea udaktari ili kuweza kuwasaidia wagonjwa.
Comments
Post a Comment