WANAFUNZI 14 WAZIMIA KWA RADI TENA BUKOMBE


Na, Ernest Magashi

Wanafunzi 14 wanezimia baada ya radi kupiga shule ya sekondari Buganzu iliyopo kata ya Uyovu wilaya ya Bukombe Mkoani Geita. 

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Paskas Muragili amethibitisha kutokea kwa tukiohilo Machi 12 saa 8:00 mchana wakati wanafunzi wa kiwa darasani wakiendelea na masomo. 

Muragili amesema awali walizimia wanafunzi watatu wakakimbizwa hospitali ya Wilaya kata ya Uyovu badae wakaaguka wanafunzi watano wakakimbizwa hospitali tena wakazimia wanafunzi sita halihiyo ilikuja baada ya kuona wezao wanachukuliwa na gari ya kubeba wagonjwa. 

"Wanafunzi watatu ndo wali patwa na hali mbaya walikimbizwa hosipitali, wakazimia watano badae wakaongezeka sita wanafunzi 11 halizao hazikuwa mbaya walizimia tu", amesema Muragili. 

"hawajapatwa na moto wa Radi kama wanafunzi wa Businda sekondari ambao ilijeruhi wanafunzi zaidi ya 80 na kupelekea wanafunzi Saba kupoteza maisha hawa wamepatwa mshituko tu na kwa sasa wamesha patiwa huduma na wameruhusiwa kwenda nyumbani", amesema Muragili. 

Ametaja chanzo cha tukio hilo nimvua iliyokuwa imeabatana na Radi hata hivyo Serikali imeedelea kutoa Elim kwa wananchi kuchukua tahazari kwenye ma tukio ya Radi licha ya Serikali kuwa na mikakati ya kuweka vifaa vya kuzuia  radi mashueleni, vituo vya afya, na kuhamasisha kwenye nyumbani za ibada ziwekewe vifaa hivyo. 

Muragili amewaomba wananchi kuondoa hifu kwenye tukio hili kuwa wanafunzi wamekufa nijambo la Kumshukru Mungu wanepata mshituko tu ukiondowa wale watatu ambao walizimia na halizao zilionekana kuwa mbaya wanafunzi wengine 11 walizimia wakihofia wezao wamekufa kwa radi. 
 
 
 

Comments